BASATA LATEKELEZA AGIZO LA MWAKYEMBE, DUDUBAYA AONJA JOTO OYSTERBAY POLISI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 28 February 2019

BASATA LATEKELEZA AGIZO LA MWAKYEMBE, DUDUBAYA AONJA JOTO OYSTERBAY POLISI

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MWANAMUZIKI wa miondoko ya Bongofleva  Godfrey Tumaini a.k.a ‘Dudu Baya' anashikiliwa na  jeshi la polisi katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Michuzi Blog Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu ameweka wazi kwa sasa Dudubaya anashikiliwa kwa mahojiano.

Hii ni kufatia agizo alilolitoa jana  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa (BASATA) kuhakikisha linamchukulia hatua kali Dudu Baya.

Pia Mwakyembe aliweka wazi sababu za kumchukulia hatua mwanamuziki huyo kutokana na makosa ya kumkashifu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji (Clouds Media Group) Marehemu Ruge Mutahaba.

Baada ya amri hiyo, Basata na jeshi la polisi limeweza kumfikisha Dudu Baya kituo cha polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Sanjari na hilo Mwanamuziki huyo anakabiliwa na kwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad