HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 4 January 2019

ZAHERA AMPA RUNGU LA UNAHODHA IBRAHIM AJIB

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga Zahera Mwinyi amemteua mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib kuwa nahodha akichukua nafasi ya beki kisiki Kelvin Yondani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Yondani kuchelewa kuripoti mazoezini bila kutoa taarifa yoyote  na kuonesha utovu wa nidhamu akiwa kama kiongozi uwanjani.

Zahera amechukua hatua hiyo baada ya Yondani kutoonekana mazoezini licha ya wenzake wote kuanza mazoezi.


“Haiwezekani unatoa siku tano za mapumziko, mtu hatokei na hakuna taarifa yoyote. Sipendi hii tabia nimemtoa Yondani, nahodha mpya sasa atakuwa ni Ibrahim Ajibu,” alisema.

Ajibu anakuwa nahodha wa Yanga kwa mara ya kwanza baada ya kupendekezwa leo hii na Kocha wa timu hiyo  Zahera akiamua  kumng’oa Yondani kwa madai ya utovu wa nidhamu.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad