HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 4 January 2019

LIGI KUU TANZANIA BARA (TPL) MZUNGUKO WA PILI KUANZA WIKIENDI HII

Afisa MtendajI Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BODI ya Ligi imetangaza kuendelea kwa lii  Kuu Tanzania Bara (TPL)  wikiendi hii kwa mzunguko wa pili kuanza kwa raundi ya Ishirini (20) kuchezwa kwenye viwanja tofauti

Akitolea ufafanuzi huo, Afisa MtendajI Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa ligi itaendelea kwa zile timu zilizosalia baada ya zingine kwenda kwenye michuano ya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

Wambura amesema kuwa, kuna timu tayari zimeshamaliza raundi ya kumi na tisa (19) kwa mzunguko wa kwanza na wao wataendelea na mzunguko wa pili wa ligi kwa ingawa kuna timu zingine zina mechi hadi tano hawajacheza.

"Kuna timu zina mechi hadi tano hawajacheza ila hatuwezi kusimamisha ligi hadi hao wengine wacheze, tutakachokifanya ni kuwapangia ratiba zao pindi watakaporejea kutoka kwenye michuano ya Mapinduzi,"amesema Wambura.

Amesema, kuwa kuna ratiba za mechi zimeondolewa kwa muda huu wakati baadhi ya timu zikiwa zinashiriki michuano ya Mapinduzi ila kama zitarejea mapema basi ratiba yao ya Ligi itaendelea kama kawaida.

Wambura ameeleza kuwa kwa msimu huu kwa zile timu zinazoshiriki michuano ya Kimataifa, kumekuwa na na mabadiliko ya ratiba kwa upande wa CAF ilakama bodi ya Ligi watajitahidi kuweza kuzipanga ratiba ili ziende sawa na ya ligi.

 Katika ratiba ya Ligi Kuu Timu ya Simba imecheza michezo 14 akiwa na mechi tano mkononi ambazo ni Azam, Kagera,Coastal Union, Mtibwa na Biashara United , huku Yanga akiwa na mechi 18 akibakisha mchezo mmoja dhidi ya Azam huku wenyewe Azam akiwa na mechi mbili dhidi ya Yanga na Simba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad