HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 6, 2019

WAZIRI UMMY ASHIRIKI UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI KIRARE JIJINI TANGA

Ummy ambaye alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Tanga akiwemo Mkuu wa wilaya hiyo Thobias Mwilapwa ambapo alikwenda Kata ya Kirare kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya bweni hilo na zahanati ya mapojoni alipofika kwenye eneo hilo la ujenzi huo alichanganya mchanga na sarauji na baadae kuchapia ukutani.

Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali wa kilomita kumi na tano kufuata huduma ya elimu jambo ambalo linaweza kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao.

Akizungumza mara baada ya kushiriki ujenzi huo Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga alisema atashirikiana na wananchi kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili zinapatia ufumbuzi.

Alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili ziweze kupata ufumbuzi haraka na kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo kwao na jamii zinazowazunguka.

Sambamba na Waziri huyo kuchangia mabati hayo wakati huo huo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imeguswa na changamoto hiyo na kuchangia mabati 50 na saruji 70 katika ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Kirare na kushiriki kwenye shughuli za ujenzi.

Alisema atahakikisha anashirikiana na wananchi kwenye maeneo mbalimbali kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto za Afya ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwenye kujiletea maendeleo.

“Labda niwaambie tu kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dkt John Magufuli imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto mbalimbali zinapatiwa ufumbuzi hivyo endeleeni kushirikiana nayo kuweza kupata mafanikio “Alisema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga jana mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata hiyo (CCM) Mwagilo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata ya Kirare (CCM) Mwagilo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata hiyo (CCM) Mwagilo anayefurahia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameshiriki ujenzi wa bweni la Wasichana kwenye shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga ambalo litakapokamilika litawasaidia kuwaepusha na vishawishi wanavyoweza kukutana nazo wanapokwenda shuleni na kukwamisha ndoto zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad