HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 16, 2019

TAEC KUANZISHA MRADI KWA KUHIFADHI CHAKULA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akisoma moja ya kitabu alichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu Tume ya nguvu za Nyuklia Nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala alipotembelea ofisi hiyo leo kujitambulisha. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi Mkuu Tume ya nguvu za Nyuklia Nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Arusha moja ya nyaraka mbalimbalimbali zinazohusiana na TAEC. Picha na Vero Ignatus. 

Na Vero Ignatus, Arusha.
Tume ya nguvu za Atomiki nchini ipo mbioni kuanzisha mradi wa uhifadhi wa chakula kwa kutumia nyuklia (food Irradiator) ambayo itachangia kupunguza upotevu wa vyakula na biashara

Mkurugenzi mkuu wa TAEC Prof. Lazaro Busagala amesema kuwa hiyo ni mipango iliyopo kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kinu cha tafiti za nyuklia, kuzalisha dawa za kutibu saratani (Research Reactor) ambapo ikifanikiwa Tanzania itakuwa ya pili kwani kwa sasa kipo Afrika ya kusini 

Profesa Lazaro Busagala amemueleza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo leo alipotembelea ofisini kwake kujitambulisha kuwa wanatazamia kuanzisha kituo cha mafunzo ya fani ya sayansi za teknolojia ya nyuklia na kuboresha miundombinu ya udhibiti wa matumizi salama ya nyuklia. 

Amesema maeneo ambayo nchi imenufaika kwa mwaka wa fedha uliopita kwa upande wa ni sekta ya Afya, maji, kilimo na mifugo waliweza kupata jumla ya shilingi Bilioni 6.1,na upande wa mafunzo shilingi bilioni 3.2

Amesema maeneo mengine waliyofaidika kwa kutumia teknolojia ya nyuklia ni sekta ya Afya waliweza kupata mashine ya kutibu ugonjwa wa saratani iliyosimikwa mwaka jana hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam na Bugando jijini Mwanza. 

Kwa upande wa kilimo teknolojia hii ya nyuklia imeweza kuwasaidia kuongeza ubora wa mbegu kwa kutumia mionzi katika upandikizaji wa kitaalamu, na kupata mifugo bora zaidi 

'' Zanzibar teknolojia hii imewasaidia kwa kuteketeza mbung'o wote kwa kuwaasi madume ya mbung'o hivyo magonjwa yite yanayoenezwa na mbung'o Zanzibar hayapo'' 

Amezitaja changamoto zinazo wakabili ni kutofahamika zaidi kwa kazi za TAEC, uhaba wa fedha za kuleta maendeleo na manunuzi ya haraka, uhaba wa vifaa kwenye kanda, mipakani na Zanzibar pamoja na upungufu wa wafanyakazi kwa sasa jumla 108 wakati mahitaji halisi ni 215

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Elimu hiyo ya nyuklia ni vyema ikatolewa kwa wajumbe wote wa kamati ulinzi na usalama ya mkoa kwani inahisika moja kwa moja na usalama na itawasaidia katika kutekeleza majukumu yao. 

Amesema hiyo ni fursa adimu kwao kama mkoa na nchi kwa ujumla kwani itawasaidia kuangalia vitu vinavyoingizwa mipakani, mifugo, chakula na hata katika uwanja wa kimataifa wa KIA ambao Arusha nao washea kuangalia vitu vinavyoingia na kutoka. 

Gambo amesema kuwa serikali ngazi ya mkoa ipo tayari kushirikiana na TAEC katika changamoto ambazo wataweza kuzitatua huku akuwataka wasikae kimya hadi changamoto iwe kubwa ndipo waiwasilishe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad