HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 December 2018

WAZIRI MBALAWA AKAGUA MIRADI YA MAJI WILAYANI BAGAMOYO

Na  Karama Kenyunko Globu ya jamii.
SERIKALI  imesema hivi karibuni itahakikisha inamaliza kabisa tatizo kubwa la ukosefu wa maji katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani linatokana na ukosefu wa miundombinuz ya usambazaji.'
'
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema hayo leo Desemba 18.2018 alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Waziri Mbarawa pia amewahakikishia wakazi wa Kiembeni, Kata ya Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani kuwa watapelekewa majisafi na salama na mpaka sasa tayari mradi utakaogharimu Sh. Bilioni 116 uko tayari na umeanza katika eneo hilo.

amesema, katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwasasa uzalishaji wa maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam umefikia lita bilioni 14 kwa mwezi.

Amesema kufuatia tatizo hilo la usambazaji ndio maana serikali kupitia mradi wake wa tanki la bagamoyo ulioanza mwaka jana iliamua kujenga tanki la maji la lita Bil. 6 ambalo litasaidia katika usambazaji kwa maeneo yote ya Bagamoyo na vitongoji vyake  ambao unatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Waziri Mbarawa ameongeza kuwa, kwa siku jiji la Dar es Salaam lina uwezo wa kuzalisha lita milioni 502 za maji na mahitaji kwa mwezi ni lita bilioni 14, lakini changamoto ni usambazaji.

"Mfumo huu wa usambazaji maji, utabadilisha maisha ya Watanzania hususani wale wa viwandani...Umekamilika kwa asilimia kubwa na hivi karibuni utaanza kutumika," alisema Mbarawa.

Aidha amezitaja changamoto kubwa mbili wanazokutana nazo katika kutekeleza miradi ya maji kuwa, ni utaratibu wa uhakiki wa wakandarasi pamoja na kuwasimamia kuanzia mradi unapoanza mpaka pale unapokamilika.

"Awali utaratibu wa kuwapata wakandarasi uhakiki haufanyiki na mkandarasi analetwa katika mradi wananchi wanaitwa wanaambiwa mradi unaanza sasa hivi tunawafuatilia kujua vifaa alivyonavyo mkandarasi na namna anavyotekeleza mradi aliyopewa "alisema.

Awali alipotembelea mradi unaotarajiwa kutekelezwa Kiembeni 1 na 2, Profesa Mbarawa aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo kupata majisafi na salama.

"Kila mtu atapata maji, hata kama upo Km 50 utapata maji. Mradi huu utagharimu sh. Bilioni 116 na tukatika utaratibu wa kumpata mkandarasi, lakini niwaombe mtakapo unganishiwa maji mlipe bili kwa wakati na muwe walinzi wa miundombinu ya maji," alisema.

Kwa upande wake Meneja Dawasa Mkoa wa Bagamoyo, Alex Ng'wandu alisema awali walikuwa wanahudumia wateja 8500 lakini kupitia mradi huo mpya wa uzalishaji maji wataongeza wateja 1500 huku wakitarajia kuondoka kwa mgao wa maji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Bagamoyo, walisema tatizo  la upatikanaji wa maji safi ni la muda mrefu na limekuwa likiwasababishia  watoto wao kupatwa na magonjwa tumbo hasa ya kipindupindu


Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo juu mradi mkubwa wa maji wa ujenzi wa Tanki ambao utakapoisha utamaliza kero zote za maji Katika Wilaya ya Bagamoyo mjini na vitongoji vyake, wakati wa Wizara ya kukagua miradi ya maji Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani iliyofanyika leo Desemba 18.2018 mradi huo ulioanza mwanzoni mwa mwaka jana unatarajiwa kumalizika mwaka huu mwishoni.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad