HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 11 December 2018

WATUMISHI WA UMMA MSIJIINGIZE KWENYE UTUMWA WA MIKOPO YA TAASISI ZISIZO HALALI-WATARA

WATUMISHI wa Umma wametakiwa kuacha kujiingiza katika mikopo inayowasababisha kuuza uhuru wao na kuwa watumwa kwa wakopeshaji wasio halali na ambao hawajasaliwa na Serikali. Kauli hiyo imetolewa wilayani Nzega na Igunga na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara wakati wa vikao vya majumuisho na Watumishi wa Wilaya hizo.

Alisema baadhi ya wanawakopesha hawakusajiliwa na hawalipi kodi za Serikali na hivyo kuendesha biashara hiyo kinyume cha Sheria na taratibu za nchi. Waitara alisema wakopeshaji hao wamekuwa wakikopesha kwa riba kubwa ambazo zimewafanya baadhi ya watumishi kuishi maisha magumu yaliyojaa utumwa ndani yake.

Alisema baadhi ya watumishi ambao ukopa wamekuwa wakikabidhi hata Kadi za kuchukua Fedha (ATM) kwa wakopeshaji na inapofika mwisho mwa Mwezi ndio upiga simu kwake ili waende kwenye ATM achukue fedha kwa ajili ya kulipa deni na kidogo za matumizi na baada ya hapo anarudisha kadi mdai wake.

Waitara alisema kitendo kinafanya taarifa za mshahara wa mtumishi kutokuwa siri kwake bali kuwa wazi hata kwa mkopeshaji jambo ambalo ni kuuza uhuru wake. Aliwataka Watumishi wa umma kuishi kulinga na mishahara wanayolipwa na kujiepusha na tamaa ambazo zinaweza kuwasababisha kujiingiza katika matatizo.
 Diwani wa Kata ya Mwanzoli wilayni Nzega Mathias Nyelo (mwenye Kaunda Suti nyeusi) akimwonyesha jana ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwita Waitara( mwenye suti ya kijivu) eneo la Shule ya Sekondari ya Mwanzoli linapoishi wakati kiongozi huyo alipotembelea Wilaya hiyo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara akitoa maelekezo jana kwa Mkandarasi wa Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Nzega Mji inayojengwa eneo la Kitangili mjini Nzega wakati akipokwenda kukagua mradi huo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara(aliye mbele)  akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za  Halmashauri ya Nzega Mji inayojengwa eneo la Kitangili mjini Nzega wakati akipokwenda kukagua mradi huo jana.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara(aliye suti kijivu)  akikagua jana maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika Shule shikizi ya Izimbili wilayani Igunga.
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilayani Igunga wakimsikiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara(hayupo katika picha)  wakati akiongea na watumishi wa umma jana.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara akizungumza na watumishi wa Halmashauri mbili za Wilaya ya Nzega jana wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara akiwa na wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika shule ya Sekondari ya Ziba jana baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mabweni Shule hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara akifundisha Hesabu wanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Ziba mada baada ya kumaliza kukagua mradi wa ujenzi wa Hosteli shule hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad