Serikali imewaasa wananchi kutoa taarifa za kuwepo wahamiaji wanaoishi maeneo mbalimbali nchini kinyume na sheria za nchi ili raia wema waweze kufanya shughuli za maendeleo kwa amani na salama huku ikiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuwa waadilifu katika maeneo yao ya kazi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kauli mbiu ya Uhamiaji Unaozingatia Utu
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Naibu Waziri Masauni amesema ni lazima wananchi washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wahamiaji haramu wanaoishi maeneo mbalimbali nchini.
“Serikali ya Tanzania inaheshimu haki za kila mtu na ndio maana tumeingia mikataba mbalimbali ya kimataifa yenye kulinda utu wa kila raia awe raia au mgeni aliyepo nchini, lakini hatutokuwa tayari kuona wahamiaji wasiofuata sheria za nchi wakiingia nchini kinyume na taratibu zilizowekwa,” alisema Masauni
“…. Nawasihi wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wageni wanaoingia nchini kinyume na utaratibu kwani wakiwaacha wanaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini.” Aliongeza Masauni.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amesema Idara yake itaendelea kutumia teknolojia katika kuendesha shughuli za uhamiaji lengo ikiwa kudhibiti uhalifu na kuiongezea mapato serikali huku akiahidi kuzuia na kudhibiti wahamiaji wanaoingia nchini kinyume na taratibu
Siku ya Maadhimisho ya Wahamaji Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Disemba 18 huku Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni “Uhamiaji Unaozingatia Utu”
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akisikiliza maelezo juu ya historia ya mabadiliko ya Pasi za
Kusafiria kutoka kwa mtaalamu wa pasi hizo, Sajini wa Uhamiaji,
Vedasto Rweikiza(kulia), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini
yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es
Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu. Kushoto ni
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akipokea zawadi kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Salma
Panja(kulia), baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo
kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,
jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu.
Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), wakiangalia
pasi ya kusafiria walipotembelea mabanda ya maonyesho wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo
kwa hapa nchini yamefamyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,
jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya
Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefamyika leo, katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa
Uhamiaji Unaozingatia Utu.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akizungumza wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo
kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,
jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia
Utu..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Dkt. Anold Kihaule,
akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa pasi za kusafiria, Sajini
wa Uhamiaji, Vedasto Rweikiza (kulia), wakati wa Maadhimisho ya
Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini
yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es
Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu.
No comments:
Post a Comment