HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 18, 2018

JESHI LA POLISI LAFANIKIWA KUMUOKOA MTOTO MCHANGA MKOANI MWANZA



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kutumia kikosi chake kabambe na jasiri, tumefanikiwa kumuokoa mtoto mchanga mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja hadi tatu aliyekua ametupwa na kuachwa bila msaada na mwanamke/mtu asiyefahamika huko mtaa wa Mwambani Wilayani Ilemela, kitendo ambacho ni kosa la Jinai.

Tukio hilo la kikatili limetokea tarehe 17.12.2018 majira ya saa 20:30hrs usiku, hii ni baada ya mtoto huyo kufungwa nguo mwilini mwake kisha kutupwa bila msaada wa aina yoyote. Ndipo kikosi chetu cha askari kilichokuwa doria chenye umakini wa hali ya juu kilipata taarifa na kufanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kumkuta mtoto huyo akiwa hai akilia sana akiwa ametupwa uwanjani hapo na mwanamke/mtu asiyefahamika. 


Baada ya Mtoto huyo kuokolewa amepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na uhifadhi, hali yake inaendelea vizuri. Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza, tunaendelea na upelelezi pamoja na msako mkali wa kumtafuta mwanamke/mtu aliyehusika katika kutenda ukatili huu ili aweze kukamatwa na kufikishwa  katika vyombo vya sheria, ili baadae iwe fundisho kwa wengine.

Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa onyo kwa baadhi ya wanawake wenye tabia kama hizi za kinyama kuwa waache kwani ni kosa la jinai lakini pia ni kinyume na haki za binadamu. Hivyo endapo mtu atabainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 
Vilevile tunawaomba wananchi pindi wanapomwona jirani yake ni mjamzito alafu baada ya muda ghafla ujauzito wake unapotea na mtoto haonekani watoe taarifa polisi ili tuweze kujiridhisha juu ya usalama wa mtoto.

Imetolewa na;
Jonnathan Shanna – ACP
Kamanda wa Polisi (M) Mwanza.
18 December, 2018.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad