HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 19, 2018

WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA WAAGIZWA KUONDOA VICHAKA VINAVYOKARIBISHA PANYA MASHAMBANI

NA TIGANYA VINCENT
WAKULIMA wa Pamba wilayani Igunga wameagizwa kuhakikisha wanasafisha na kuondoa vichaka na magugu yaliyopo kando kando mwa mashamba yao ili kuhakikisha panya na wadudu waharibifu hawageuzi maeneo hayo kuwa maficho na kuingia mashambani kwa ajili ya kula mbegu zilizopandwa.

Kauli hiyo imetolewa jana wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiwa katika ziara yake ya kuelimisha na kuhamasisha wakulima wa zao la pamba kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo baada ya baadhi ya wakulima kudai uwepo wa panya wanaoshambulia mbegu za pamba walizopanda.

Alisema wadudu na panya ambao wameanza kuingia katika mashamba ya wakulima na kushambulia mbegu ambazo  wamepanda wanatokea katika vichaka vichaka vilivyoachwa kando kando ya mashamba hayo. Mwanri alisema wakati juhudi za kuwasiliana Wizara ya Kilimo ili kupata dawa ya kuwaangamiza panya na wadudu hao wanaoshambulia mbegu zilizopandwa ni vema wakulima wakahakikisha mashamba yao ni masafi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza Maafisa Ugani kuhakikisha wanahamia vijijini kwa ajili kusaidia wakulima kutafuata njia za awali za kukabiliana na tatizo hilo na kuokoa mazao yao ili wasikate tamaa. Kwa upande wa Afisa Kilimo , Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Igunga (DAICO) Erasto Konga alisema wakulima wamesha ripoti kwao uwepo wa tatizo la panya na wadadu wanaoshambua mbegu zilizopandwa na wakulima wamesharipotiwa wamesharifikisha kwenye Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kuwapatia dawa za kuwaua.

Alisema taratibu za manunuzi zinaendelea ili kupata dawa hiyo haraka kwa ajili ya kuokoa mazao ya waakulima. Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameagiza kila mkulima mkoani humo kuhakikisha analima ekari tatuu za pamba ili kuongeza malighafi kwa ajili ya viwanda vilivyopo na vinavyotarajiwa kujengwa.

Alisema agizo hilo ni azimio ambalo Mkoa wa Tabora umefikia ili kuhakikisha kunakuwepo na malighafi nyingi kwa ajili ya viwanda. Ziara ya Mkuu wa Mkoa itaendelea katika Wilaya za  Nzega , Uyui , Urambo na Kaliua ili kuwaelimisha wakulima wa pamba.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa elimu ya kanuni 10 za kilimo bora cha pamba jana katika Kijiji cha Kitangile wilayani Igunga. Kijiji hicho ndio mara ya kwanza kinaanza kulima zao hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa elimu ya kanuni 10 za kilimo bora cha pamba na umuhimu wa kung'oa maotea ya msimu uliopita jana katika Kijiji cha Mwabakima  wilayani Igunga. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akionyesha baadhi ya maotea yaliyokutwa katika shamba la mmoja wa wakulima wakati akitoa maelezo juu ya kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo jana katika Kijiji cha Mbutu wilayani Igunga.
.Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Choma cha Nkola wilayani Igunga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha ) wakati akitoa maelezo juu ya kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo jana  wilayani Igunga ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha kilimo cha pamba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad