HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 December 2018

JESHI LA MAGEREZA LAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO (2019-2023) DHIDI YA HIV/AIDS NA TB

Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza Augustine Mboje,ambaye alimuwakilisha Kamishna Jenerali wa Magereza, akifungua kikao cha Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB kwenye ukumbi wa kivukoni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 18 December 2018. Aliyekaa ni Kamishna wa Mafunzo Zanzibar, Ally Abdala.
Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar, Ally Abdala akichangia mada kwenye mjadala wa Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV, AIDS na TB.
Daktari Fulgency Binagwa akitoa semina ya Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB kwenye ukumbi wa kivukoni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Daktari Peter Mfisi akitoa semina kwa wadau waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB kwenye ukumbi wa kivukoni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza Augustine Mboje,ambaye alimuwakilisha Kamishna Jenerali wa Magereza (wa tatu toka kulia) akikata utepe kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB.
Naibu Kamishna Jeremia Katungu akitoa neno la shukrani kwa wadau wa Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB. Aliyeketi ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi Musa Kaswaka.
Afisa Mradi Kitaifa wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayopambana dhidi ya madawa ya kulevya na uhalifu Bi. Immaculate Nyoni akimshukuru  Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza Augustine Mboje kwa kuzindua Mpango Mkakati dhidi ya HIV,AIDS na TB.
 Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza Augustine Mboje (wa tatu toka kushoto,walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliowezesha kukamilika kwa Mpango Mkakati wa miaka mitano dhidi ya HIV,AIDS na TB katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Jeshi la Magereza

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad