HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 12, 2018

Serikali yaipongeza Xprize Foundation kwa kuonesha njia ya kusaidia watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham mara baada ya kuwasili katika ofisi za mkoa wa Tanga mwishoni mwa juma wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE mkoani humo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za mkoa wa Tanga wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE mkoani humo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za mkoa wa Tanga wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE mkoani humo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos, Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham pamoja na Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert  wakipokea taarifa fupi kwenye ofisi za Kaimu Katibu Tawala wa  mkoa wa Tanga Bi Monica Kinanan kabla ya kuelekea kukagua mradi wa XPRIZE uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham pamoja na Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert mara baada ya kuwasili kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga kukagua mradi wa XPRIZE.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (kulia), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos(kushoto) wakipata maelezo ya kifaa maalum kinachotumia umeme wa jua kuchajia Vishkwambia kutoka kwa Mtaalamu wa Tehama wa mradi wa XPRIZE Tanga, Bw. Xavery Njovu wakati wa ziara ya kukagua mradi huo uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akiangalia jinsi mmoja wa watoto wa kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga walio nje ya mfumo rasmi wa elimu anavyojifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia Vishkwambi hiyvo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham wakitazama jinsi watoto wa kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga walio nje ya mfumo rasmi wa elimu wanavyojifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia Vishkwambi hiyvo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE mkoani humo mwishoni mwa juma.
 Baadhi ya watoto wa jamii ya kifugaji walio nje ya mfumo rasmi wa elimu wa kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wanaonufaika na mradi wa XPRIZE wakitumia Vishkwambi kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia programu zilizomo ndani ya Vishkwambi hivyo walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham (hawapo pichani) mwishoni mwa juma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi –Elimu Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Bi. Odilia Mushi (kulia) wakimtamzama mmoja wa mtoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu Sophia Ibrahimu (11) akijifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia programu zilizomo ndani ya Vishkwambi wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Mkurugenzi Msaidizi –Elimu Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Bi. Odilia Mushi (kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Elimu cha UNESCO, Faith Shayo (kushoto) wakimtamzama mmoja wa mtoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu Neema Saitoti (11) akijifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia programu zilizomo ndani ya Vishkwambi wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi –Elimu Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Bi. Odilia Mushi (kulia) wakimtamzama mmoja wa mtoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu Elias Silas Roti (11) akijifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia programu zilizomo ndani ya Vishkwambi wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akimtamzama mmoja wa mtoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu Joshua Michael (7) akijifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia programu zilizomo ndani ya Vishkwambi wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Kamati wa Kitaifa ya mradi wa XPRIZE ikijumuisha UNESCO, WFP, Wizara ya Elimu pamoja na  TAMISEMI wakishiriki mkutano wa kutoa ripoti ya maendeleo ya mradi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Tanga mara baada ya kukagua mradi katika moja ya vijijini mkoani humo.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (kulia) kufungua rasmi kikao cha Kamati ya kitaifa ya mradi wa XPRIZE kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Tanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akifungua kikao cha Kamati ya Kitaifa ya mradi wa XPRIZE kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Tanga mwishoni mwa juma. Katikati ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos na kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Bi. Monica Kinana.
 Sarah Hulbert kutoka WFP akiwasilisha taarifa ya mradi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kamati ya kitaifa ya mradi wa XPRIZE mara ya Katibu Mkuu kukagua mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Elimu cha UNESCO, Faith Shayo.
 Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Bi. Elianne Philibert akizungumzia hatima ya mradi huo wakati wa kikao cha Kamati ya kitaifa ya mradi wa XPRIZE kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Tanga.
 Mtaalamu wa Tehama wa mradi wa XPRIZE Tanga, Bw. Xavery Njovu akitoa taarifa ya mradi wakati wa kikao cha Kamati ya Kitaifa ya mradi huo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mkuu wa kitengo cha Elimu cha UNESCO, Faith Shayo akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kitaifa ya mradi wa XPRIZE kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Tanga.

Na Mwandishi wetu, Tanga
SERIKALI imepongeza mradi wa XPRIZE kwa kuonesha njia nyingine ya kuwapatia elimu ya kusoma, kuandika na kuhesabu watoto wengi walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wakati alipotembelea wilaya ya Mkinga, ikiwa ni mojawapo ya wilaya sita (6) za Mkoa wa Tanga, zinazonufaika na mradi huo. 
Akizungumza katika mahojiano, Katibu Mkuu huyo alisema kwamba kinachowaondoa watoto wengi katika masomo si lazima iwe mimba kwani wapo watoto wengi hasa wakiume ambao wanakimbia majumbani na kukosa haki yao ya msingi ya elimu.
“Huu mradi umetuonesha njia nyingine kabisa ya kukabiliana na tatizo hili. “ anasema Dk Akwilapo ambaye amesema ni sera ya serikali ya kuhakikisha kwamba watoto wote hata wale ambao hawakuingia katika mfumo rasmi wanaingiza katika mfumo wa elimu kwa kupitia taratibu mbalimbali. Miongoni mwa taratibu hizo ni utaratibu wa MEMKWA kwa elimu ya msingi na MESPA kwa sekondari. Alisema mradi huo wa MEMKWA umeonesha matokeo mazuri kwa sasa kwani tayari watoto 800 wamefikishwa katika shule wakafanyiwa mitihani na kuingizwa kuendelea na madarasa ya pili.
Mradi wa XPRIZE ambao utamalizika mwaka kesho ukitumia vishkwambi katika mafunzo kwa watoto waliokosa elimu ya msingi kufikia miaka 9, ni mradi wa dunia ambapo teknolojia inajaribiwa kusaidia wale waliokosa nafasi ya kuingia shule.
Akizungumzia hatima ya mradi huo, Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert  alisema kwamba mafanikio yake yatawezeshwa kutengenezwa kwa moduli za kufundishia watoto walio nje ya mfumo rasmi wanaotumia lugha ya Kiswahili.
Alisea mradi huo wa kutumia vishikwambi kufundisha watoto kwa kutumia programu za kujifunza unahusisha nchi kadhaa na baada ya kukamilika mwakani matokeo yake yatawekwa wazi na hivyo teknolojia kujulikana inavyoweza kutumika kupeleka mafunzo kwa waliokosa elimu rasmi.
Imeelezwa kuwa mradi utakapokamilika mwakani utakuwa umewatoa kimasomaso wanafunzi 2,697 katika vitongoji 170 vinavyofanyiwa mradi huu wa majaribio.
Vishkwambi hivyo vinachajiwa kwa kutumia nishati jadidifu ya jua katika maeneo maalumu yaliyotengenezwa kwa ajili ya kuzichaji.
Mradi huo wa XPRIZE unaotumia ubunifu wa teknolojia unafanyika chini ya uangalizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Kamati ya kitaifa inayohusisha pia Wizara ya Elimu na TAMISEMI. Lengo kuu baada ya mradi huo kukamilika ni kuwapata watoto ambao wataweza kuingizwa darasa la pili na kuendelea na pia kuongeza uwezo wa kumudu masomo kwa watoto wa darasa la pili.
Mkuu wa kitengo cha Elimu cha UNESCO, Faith Shayo alisema kwamba mradi huo unalenga kuchanganua kama inawezekana kwa watoto walio nje ya mfumo rasmi wa Elimu kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kwa kutumia vishkwambi. Aliongeza kuwa mradi huu uko chini ya shindano ya Global Learning XPRIZE yanayodhaminiwa na Taasisi ya XPRIZE Foundation ya Marekani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad