HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 4 December 2018

Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, imesaini mkataba wa Bilioni 6.2 kwa ajili ya ujenzi wa jengo kisasa la Utawala la Halmashauri hiyo litakalojengwa na wakala wa Majengo Nchini (TBA). Akizungumza wakati wa utiaji saini ujenzi wa jengo hilo la Utawala leo jijini Dar es Salaam, Meya Jacob amesema ni matarajio yake ujenzi huo utakamilika kwa wakati kama walivyopanga katika kuondokana na ofisi za kupanga

Amesema Serikali Kuu ilitoa mwongozo wa kuhakikisha wanawatumia TBA katika mradi huo lakini angekuwa yeye binafsi angependekeza kushindanisha wakandarasi kadhaa wakiwamo Suma JKT ili kupata mkandarasi mwingine. "Naomba nitoe tahadhali kwa TBA mkajipime kabl hamjaanza ujenzi huu kwani mkionyesha kusuasua mimi ndio ntakuwa wa kwanza kulalama kwa vile wadau wetu wa pili wa mradi huu ambao ni Serikali wamewateua nyie mjitahidi msiwaangishe ili kuendelea kuwa na imani na nyie" amesema Jacob.

Aliweka  angalizo hilo kwa sababu ya historia fupi ya TBA kwenye baadhi ya mikoa ambapo wameshindwa kutekeleza mikataba na kusababisha mingine kunyang'anywa. "Tumeskia huko mikoani baadhi ya miradi mliporwa kwa sababu ya uzembe wa watendaji wenu wa huko lakini kwa hapa Dar ea Salaam hamjapata kashfa hiyo hivyo naomba mjipange vyema katika mradi huu kwa kufanya kuwa na jengo,"alisema Jacob.

Amesema mradi huo utekelezwaji wake hadi ukamilike utatumia jumla ya Sh. BIlioni 6.2 ambapo Serikali Kuu itatoa Sh.Bilioni.4.3 na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani Sh.bilioni 1.9. Jacob amesema Ubungo ina.watumishi 4300 ambapo imekuwa ikilazimika kwa sasa kukodi jengo la halmashauri hiyo kwa kiasi cha Sh.milioni 192 kila mwaka.

Amesema katika miaka hii miwili tayari tumepoteza  Sh.milioni 400 kwa ajili ya kupanga jengo jambo ambalo linasababisha kupoteza fedha nyingi za halmashauri ambazo zingetumika katika huduma za kijamii," alisema Jacob.Amesema angependelea zaidi mradi huo badala ya kutumia.mwaka mmoja kukamilisha ujenzi ni vyema ukatumia hata.miezi tisa kwakuwa fedha zipo na wanahitaji haraka jengo hilo ili kuokoa fedha za walipa kodi.

Jacob amesema hakuna haja kutokusaini.mkataba huo kwa sababu umezingatia masharti yote pamoja na vifungu muhimu. Aidha amesema halmashauri hiyo ina  awali wananchi wake walikuwa wakitembea kilometa 30 kwenda kupata huduma lakini kwa sasa kusogea kwa huduma hiyo itasababisha kutembea kwa kilometa nane  hadi 10. Alisisitiza mradi huo kusaidia kuinua uchumi wananchi wake kwa kutoa ajira na kununua vifaa mbalimbali vya ujenzi ndani ya halmashauri hiyo.

Aliipongeza Serikali kwa kutoa kiwanja hicho ambacho awali halmashauri hiyo ilitakiwa wakinunue kwa bilioni mbili ambapo Serikali imewapa bure. Kwa upande wake,  Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam, Edwin Godfrey alisema,  amepokea salaam za watendaji wa halmashauri hiyo na kujionea mazingira halisi ya kazi.

Alisema atahakikisha wanafanyakazi kwa weledi iwe jua, mvua au sikukuu watakuwa eneo la kazi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati na kiwango kinachotakiwa. "Tumepokea maagizo yote tunachoahidi ni iwe nvua, jua, usiku, sikukuu tutafanyakazi masaa yote kwa kiwango kinachohitajika ambacho kipo kwenye mikataba yetu,"alisema Godfrey.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,  Beatrice Kwai alisema, atahakikisha anasimamia.mkataba ili.utekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa. Alisema kama halmashauri wamejipanga kutoa malipo ya gharama za.mradi huo ili utekelezwe kwa wakati. "Mkataba huu.umesainiwa.leo (jana ), ninachoomba kama.mkandarasi anatakiwa awe eneo la.kazi ahakikishe abatimiza wajibu wake,"alisema  Beatrice.
 Mkuregenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai(kulia) na  Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA)  Mkoa wa Dar es Salaam, Edwin Godfrey(kushoto) wakibadilishana hati za  makubaliano ya ujenzi  ofisi ya manispaa hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob akizungumza na waandishi habari mara baada kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuregenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai na kushoto ni Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA)  Mkoa wa Dar es Salaam, Edwin Godfrey.
TBA na Manispaa ya Ubungo wakisaini Mkataba ya makubaliano ya ujenzi wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai akizungumza na waandishi habari namna waliyojiwekea mazingira ya ujenzi wa Manispaa hiyo wakati wa kuliliana saini na TBA.
Picha ya pamoja ya watendaji na Manispaa ya Ubungo na TBA na baadhi ya Madiwani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad