Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk amesema wananchi wengi wanashindwa kupata huduma za msaada kisheria kutokana na kukosa uelewa wa kupata watoa huduma za msaada wa Kisheria. Groenendijk ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana kwa jina la "Siyo Tatizo" inayolenga kuongeza ufahamu kwa jamii kuhusiana uwepo wa upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa Kisheria , amesema jamii imezungukwa na matatizo yanayotokana na kukosa msaada wa kisheria na kufanya kukosa haki zao.
Groenendijk amesema Kampeni hiyo ni kuongeza ngumu ya uelewa kwa jamii juu ya upatikanaji wa huduma ya bure za msaada wa kisheria zitolewazo na wasaidizi wa kisheria. "LSF Tanzania kwa dhati inalenga kuleta unafuu zaidi hasa kwa wanawake wenye hali ngumu ambao haki zao za msingi zimepewa zikifinywa au kukosekana kutokana na sababu mbalimbali hali hiyo imechangiwa zaidi na ukosefu wa usaidizi wa kisheria" amesema Groenendijk. Amesema kuwa kampeni hiyo watawafikia wananchi wote katika kampeni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Siyo Tatizo Tena ya upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa kisheria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miradi wa LSF Scholastica Tully akizungumza kuhusiana kampeni ya kutoa huduma kuhusiana na upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa kisheria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana kwa jina la Siyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Mwasiti Almas akizungumza kuhusiana na kutoa elimu ya upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa kisheria katika uzinduzi wa LSF iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Lameck Ditto 'Dogo Ditto' akizungumza jinsi atavyohamasisha kuhusiana na kampeni ya kutoa huduma za bure za msaada wa kisheria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana kwa jina la Siyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk(wa kwanza kulia) akipeana mkono na Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Mwasiti Almas wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana kwa jina la Siyo inayohusuUpatikanaji wa Huduma za bure za msaada wa kisheria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment