HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 14 December 2018

Kihanda:Wahasibu wana nafasi muhimu katika maendeleo ya viwanda

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
MKUU wa Taasisi ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Joseph Kihanda amesema kuwa wahasibu wanaozalishwa nchini waangalie   katika kutumika uchumi wa viwanda. Kihanda ameyasema hayo leo katika kongamano la pili la Taasisi hiyo,  amesema kuwa kongamano la kuelekea mahafali ya Chuo hicho ni wahadhiri kuwasilisha tafiti mbalimbali ya kuweza kuafanya wanafunzi na wahitimu kupata vitu vya ziada kufanya.

Amesema kuwa tafiti huaza chini ambazo zinafanya wahitimu kuwa wabobezi katika masuala mbalimbali yanayoendana na taaluma yao katika kusaidia maendeleo ya nchi. Dkt.Kihanda amesema kuwa changamoto iliyopo  kwa wahasibu nchini ni kutotosheleza mahitaji hivyo kama taasisi wajibu wa kuzalisha wahasibu wengi katika kuziba pengo lillopo nchini.

Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Majule amesema kuwa watalaam wafanye tafiti za kuiletea maendeleo nchi na sio za kupanda cheo huku jamii yako haijaweza kufaidika na wahasibu lazima wajenge mazingira ya uadilifu katika kufanya kazi na kuleta maendeleo ya nchi
 Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu nchini (TIA) Dkt. Joseph Kihanda akizungumza katika kongamano la wanafunzi kwa wahadhiri wa kuwasilisha mapachapisho ya uatafiti, jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Amos  Majule akitoa chapicho katika kongamano la wanafunzi wa TIA lilofanyika katika Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri wa Chuo Kuu  cha  Kilimo SUA Dk. John Jackonia akitoa mada katika utafiti alioufanya katika kongamano la Taasisi ya Uhasibu Nchini TIA lilofanyika katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri wa Taasisi ya  Uhasibu Tanzania, Kelvin Njunwa akitoa mada katika kongamano la Taasisi ya Uhasibu Nchini TIA lilofanyika ukumbi wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye kongamano lilofanyika ukumbi wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad