HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 21, 2018

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye kikao cha kwanza na Watumishi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mnyepe aliwataka Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa kufuata miongozo na kutekeleza majukumu yao kwa bidii, weledi na uzalendo. Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Savera Kazaura. 

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Savera Kazaura akizungumza wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018. Kulia ni Katibu Mkuu, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi(kulia) akichangia jambo wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani).



Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad