Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva (katikati) akionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega wakishiriki. Kampeni hiyo inaendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva (wa pili kushoto) wakionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba.
Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva (katikati) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo viwanja vya Zakheim.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo viwanja vya Zakheim.
Chege Chigunda akifunga kazi kwa mashabiki wake katika fainali za burudani na kampeni Wilaya ya Temeke.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akimtuza msanii Chege Chigunda alipokuwa akifunga kazi katika fainali za burudani na kampeni hizo.
Msanii Shilole aka Shishi Baby akitikisha kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga wilayani Temeke.
Umati wa wananchi ukifuatilia burudani katika uzinduzi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga wilaya ya Temeke.
Msanii Man Fongo jukwaani akiwaburudisha wapenzi wa miondoko ya Singeli katika kampeni hizo zilizomalizika kwenye Uwanja wa Zakhein.
Msanii Man Fongo (kushoto) jukwaani akiwaburudisha wapenzi wa miondoko ya Singeli katika kampeni hizo.
No comments:
Post a Comment