HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 4, 2018

KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KIKAZI GEREZA KONDOA NA KING’ANG’A MKOANI DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akisalimiana na maafisa wa gereza la mifugo King’ang’a wilayani Kondoa mkoani Dodoma mara baada ya kuwasili gerezani hapo alipofanya ziara ya kikazi Desemba 3, 2018. 

Na ASP Deodatus Kazinja, Kondoa

Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza nchini watakiwa kujenga uhusiano mwema na viongozi wa kada tofauti tofauti nje ya Jeshi la magereza kwa lengo kuleta mshikamano na ushirikiano wa kiutendaji. Wito huo uliotolewa Desemba, 3 mwaka huu na Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na maafisa na askari wa magereza ya King’ang’a na gereza Kondoa wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Kamishna Kasike alisema kiongozi au askari wa magereza anayejifungia katika eneo lake tu ni vigumu kuwa na ushirikiano ulio mzuri na viongozi wenzake jambo ambalo lawezakukwamisha baadhi ya mambo ya kiutendaji ambayo yangetatulika kirahisi kama kungekuwa na uhusiano mzuri. “ Ukiwa kiongozi au askari wa kawaida jitahidini kutambua viongozi, watumishi wenzenu na jamii inayowazunguka, jenga nao uhusiano ulio mwema. Hakuna anayejitosheleza kwa kila jambo. Sote tunahitajiana kwa njia moja ama nyingine” alisisitiza CGP Kasike.

Kwa upande mwingine, CGP Kasike aliwataka maafisa na askari wote wa magereza nchini kudumisha nidhamu kazini. Alisisitiza kuwa nidhamu ndiyo nguzo kuu ya uaskari na nidhamu ndiyo chimbuko la utendaji ulio bora mahala pa kazi.

Aidha, Jenerali Kasike aliwafahamisha maafisa na askari katika magereza hayo kuwa maagizo ya Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ya kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa yanaendelea vizuri na kwa kuanzia tayari magereza 10 yameanishwa.

“Ninayo furaha kukufahamisheni kwamba katika agizo la kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa tayari magereza 10 yatakayozalisha mahindi, mpunga na maharage yameainishwa. Tunachokifanya sasa ni kutoa kipaumbele cha raslimali chache tulizonazo zielekee katika magereza hayo” alifahmisha CGP Kasike.

Kamishna Jenerali Kasike aliwataka maafisa na askari wote nchini kuwa wavumilivu na wastahimilivu wakati changamoto mbalimbali zinazowakabili wao binafsi na jeshi kwa ujumla zinatafutiwa ufumbuzi kwa zote serikali inazitambua na anayo matumaini kuwa zitatatulika hatua kwa hatua.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (mwenye miwani) akikagua maeneo ya mipaka ya gereza la mifugo King’ang’a inayodaiwa kuvamiwa na wananchi mbalimbali wakifanya shughuli za kilimo na ufugaji ndani ya eneo la gereza. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa gereza hilo Mrakibu wa Magereza Josephat Mkama.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akikagua mradi wa tofali za kuchoma wa gereza King’ang’a zilizoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari wa gereza hilo pamoja na gereza Kondoa. CGP Kasike alisisitiza kufyatuliwa kwa wingi kwa tofali hizo ili kukabiliana na uhaba wa nyumba katika vituo hivyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad