HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 December 2018

IRENE UWOYA AELEZA SABABU ZINAZOFANYA AFANIKIWE KIMAISHA


Na.Khadija seif,globu ya jamii
KATIKA kusherehekea siku yake ya  kuzaliwa Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya  amefanya dua ya  Kuwarehemu watu maarufu waliotangulia mbele ya haki.

Akizungumza wakati wa kutoa neno la shukrani kwa watu ambao wamejumuika nae kwenye sherehe hiyo ikiwemo  watu wenye ulemavu na wasiojiweza Irene amesema amefanya hivyo ili kurudisha fadhila kwa watu  ambao siku zote wamekua wakitazama kazi zake pamoja na kununua .


Uwoya ameeleza kuwa ni muhimu kuwasaidia watu wasiojiweza na kuwapatia mahitaji ili waweze kujisikia faraja na kuona wasanii wapo pamoja nao na kwa Leo ameweza Kula nao chakula pamoja na kuwapatia zawadi. "Hakuna kitu kikubwa kama fungu la Kumi kwani sio hiyari na mafanikio yangu ni kutokana na kutoa sadaka kwa wingi hakuna  uchawi wowote bali ni kufanya sadaka kwa wingi na kumuomba mwenyezi mungu "alisema Irene uwoya
Kwa upande wa Mlezi wa kituo kinachowalea watoto yatima Almadina center kilichopo Tandale Yusra Mohamed ametoa pongezi kwa Irene Uwoya kwa kuwafariji watoto hao pamoja na walemavu kwani ni wasichana wachache wenye maono kama yake kuwapa nafasi watu hao kujumuika nao pamoja .

Hata hivyo watoto wameshukru na kufurahi siku ya Leo japo imekua ni mara chache kupatiwa misaada na kusubiri siku za sikukuu. Watoto Hawa ni wa kwetu sote tuwasaidie na kushirikiana nao katika kuwalea na kuwakuza katika maadili mema na yanayompendeza mwenyezi mungu.

Pia kwa upande wa Kiongozi wa Wasanii wa filamu ambae pia ni mtu wa karibu wa Irene uwoya, Steve Nyerere amempongeza Irene kwa kujumuika na watu hao na kuwashauri wasanii wengine waige mfano na kuwaenzi na kuwaombea dua kwa wingi watu waliofanya mazuri hapa nchini .


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad