HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 3 December 2018

Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa

 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto)  akivishwa skafu na kijana wa Skauti wa Shule ya Sekondari Dodoma Vicky Jactan (Kulia) , alipowasili shuleni hapo jana Jijini Dodoma katika hafla ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa  na  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na  wataalamu wa lugha ya Kiswahili ( Hawapo katika picha),  jana Jijini Dodoma katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa  na  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma..
 Mhitimu ambaye ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Chikole ya Jijini Dodoma Bibi. Neema Mkobalo akisoma risala  kwa mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison  Mwakyembe (Wa tatu kulia) katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa  na  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia)  akimkabidhi cheti  mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi ya  wataalamu wa lugha ya Kiswahili  Mwalimu  wa Shule ya Msingi Chikowa  Bibi. Theresia Lejale jana Jijini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia)  akimkabidhi cheti  mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi ya  wataalamu wa lugha ya Kiswahili  Mwalimu wa  wa Shule ya Msingi Vikonje  Bw. Emmanuel Mzumya jana Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu  wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa  na  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,DODOMA)

Na. Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa lugha ni kielelezo na  sehemu  muhimu ya utambulisho wa taifa  lolote duniani.
Hayo ameyasema jana Jijini Dodoma  katika Hafla  ya  kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa  na  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
“Taifa lolote lisilo na utamaduni wake ni taifa mfu, na sisi tunajivunia kwa kuwa na utamaduni hai ikiwemo lugha yetu ya Kiswahili” alisema Dkt. Mwakyembe
Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa  lugha ya Kiswahili ni kitambulisho cha utamaduni wa Mtanzania , kwa kuwa ndiyo lugha inayowaunganisha watu katika shughuli mbalimbali za Kijamii, Kisiasa na kiuchumi.
Dkt. Mwakyembe anazidi kufafanua kuwa takribani lugha elfu sita (6000) huzungumzwa kila siku  duniani  ambapo  lugha ya Kiswahili  ni miongoni mwa lugha 10 zinazoongelewa kwa wingi.
“Mafunzo haya ni mwanzo tu mwa mambo mengi mazuri ambayo Wizara yangu imepanga kufanikisha na ukizingatia kampeni ya mwaka huu ya Uzalendo na Utaifa ina kauli mbiu inayohamasisha kukuza lugha yetu ambayo ni Kiswahili Utashi Wetu, Uhai Wetu” alisema Dkt. Mwakyembe.
Naye Kaimu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bibi. Consolata Mushi alieleza  kwamba mpaka sasa Baraza limefanikiwa kutoa mafunzo kwa wataalamu 350 ambapo jumla ya wataalamu wapatao 198 tayari wametunukiwa vyeti na wataalamu 98 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti hivyo mwezi Desemba 2018. 
Anazidi kueleza  kuwa  lengo la  BAKITA ni kuwapa fursa wataalamu hao  ili waweze kusajiliwa katika mfumo wa kanzi data ambayo tayari imesajili wataalamu wapatao 380 kwa ajili ya kufundisha lugha ya  Kiswahili kwa wageni ndani na nje ya nchi.
Pia Bibi. Consolata alitoa  wito kwa wataalamu wa Kiswahili kutoka katika  mikoa yote ya Tanzania Bara kujiunga na kupata  mafunzo hayo ili waweze   kuorodheshwa katika kanzi data hiyo kwa ajili ya  kukibidhaisha Kiswahili katika mataifa mengine.
Kwa niaba ya wahitimu wenzake  Mwalimu wa shule ya Sekondari Chikole ya Jijini Dodoma Bibi. Neema Mkobalo alimshukuru  Waziri Dkt. Mwakyembe pamoja na uongozi wa BAKITA kwa  kuratibu mafunzo hayo na kuahidi kufanyia kazi yale yote waliyojifunza .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad