Meneja
wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akimkabidhi, Mkuu wa
Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, moja kati ya
kompyuta tano zilizotolewa na benki hiyo leo hii kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo. Wengine ni wanafunzi wa shule hiyo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akizungumza kwenye hafla hiyo..
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akitoa taarifa ya shule hiyo kabla ya kupokea msaada huo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akimkabidhi taarifa ya shule hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.
Mwanafunzi wa shule hiyo, Suleiman Khamu, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia kompyuta walizo kabidhiwa na benki hiyo.
Mwanafunzi wa shule hiyo, Anwar Mohamed, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia kompyuta walizo kabidhiwa na benki hiyo.
Mwanafunzi wa shule hiyo, Thomson Athanas, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia kompyuta wazizo kabidhiwa na benki hiyo.Na
Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akizunguza wakati akipokea msaada huo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akizungumza kwenye hafla hiyo.
BENKI
ya NMB imetoa msaada wa kompyuta tano kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kukabidhi kompyuta hizo, Dar es Salaam leo, Meneja
wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd alisema kompyuta hizo
zitachangia kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji hasa
kipindi hiki ambacho dunia inaongea zaidi juu ya sayansi na teknolojia.
"Kompyuta
tunazozitoa leo hii ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii tunaimani
zitaweza kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi hususani kwenye masomo ya
Tehama" alisema Idd.Aliongeza kuwa kompyuta hizo tano zitasaidia
kuimarisha mafunzo ya Tehama shuleni hapo na kuongeza uelewa mzuri wa
masomo ya Tehama kwa wanafunzi wawapo shuleni na hata baada ya kumaliza
masomo yao.
Idd
alisema kuwa kompyuta hizo ni sehemu ya kompyuta 150 zinazopelekwa
mashuleni kwa mwaka huu ambapo pia katika Wilaya ya Same wamebahatika
kupata mgao wa kompyuta tano.
Akizungumzia
kuhusu benki hiyo alisema ndiyo inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi
mengi kwani ina matawi zaidi 228, ATM zaidi ya 800 nchi nzima, NMB
wakala zaidi ya 6000 pamoja na idadi ya wateja zaidi ya milioni 3 idadi
ambayo ni hazina kuwa ukilinganisha na benki zingine na kuwa imezifikia
wilaya zote kwa asimilimia 100 pamoja na kuboresha huduma za kibenki kwa
njia ya mtandao ili kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wengi.
Mkuu
wa shule hiyo, Salama Ndyetabura akipokea msaada huo alisema kwa
nyakati tofauti shule hiyo imepokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau
wa elimu yenye thamani ya sh.milioni 108,516,780 katika kipindi cha
Januari 2015 hadi Oktoba 2018.
Alisema
kwa msaada huo walioupokea kutoka Benki ya NMB, umeonesha dhamira ya
dhati katika kuunga mkono nia ya dhati ya Rais Dkt.John Magufuli ya
kutoa elimu ya msingi bila malipo yoyote kwa watanzania.
Katika
hatua nyingine Ndyetabura alisema kwamba katika kuhakikisha
wanafanikiwa kitaaluma shule hiyo ilipata wafadhili ambao waliwapatia
kompyupa tano na kuwaunganisha kwenye mkongo wa Taifa huduma ambayo
inawawezesha kupata makala na mambo mbalimbali na kufundisha kwa njia ya
mtandao ambapo ameiomba benki hiyo kuwasaidia kwa mara nyingine kupata
Projekta ambayo itasaidia kufundisha wanafunzi kwa njia ya teknolojia
kwa urahisi zaidi kufundisha masomo yote ambapo wataweza kutekeleza sera
ya elimu ya mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment