HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 24 November 2018

WANANCHI WA CHANGANYIKENI WAANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA RUVU CHINI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiwa ametembelea moja ya nyumba iliyounganishiwa maji kutoka katika mradi waupanuzi wa huduma ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka  (DAWASA).

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo ametembelea miradi ya upanuzi wa huduma ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka  (DAWASA) inayohusisha ujenzi wa matenki na upanuzi wa mtandao. 

Miradi hiyo itanufaisha Manispaa za Kinondoni na Ubungo  na Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo ukiwa unahusisha matenki matano yenye ujazo wa Lita Milioni 6.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhandisi Kalobelo amesema mradi huu ulio mbioni kukamilika umeanza kuonesha manufaa kwa wananchi wa Changanyikeni kuanza kupata maji.

Mhandisi Kalobelo amesema, matarajio ya serikali ni kuona wananchi wanapata maji safi na salama na maji ni rasilimali adimu wananchi wanatakuwa watunze miundo mbinu.

Amesema, kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wa Goba, Wazo, Changanyikeni na Salasala ya kukosa maji kwa muda mrefu ila kumalizika kwa  miradi hii mikubwa iliyowezeshwa na serikali kupitia Wizara ya Maji wananchi wataanza kunufaika baada ya kuyasubiri maji kwa muda mrefu.

" mradi huu ni wa awamu ya kwanza, kuna mradi wa pili ambao serikali tayari imepata hela kutoka Benki ya Dunia utakaowanufaisha wananchi walio maeneo ambayo hajayanufaika na mradi kwa kwanza," amesema Mhandisi.

Amesema kuanzia siku ya Jumatatu Novemba 26, tenki la maji la Changanyikeni litaanza kupokea maji na kufikia Jumatano wananchi watakuwa tayari wameshaunganishiwa maji.

Amewapongeza DAWASA  kwa jitihada wanazozionyesha kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji na ametoa rai kwa wananchi wajiunge kwenye mradi huu ili wapate maji safi na salama.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo (kushoto) akipata maelezo ya mradi kutoka Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprina Luhemeja (wa pili kushoto) akiwa sambamba  Mkurugenzi wa Maji  na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji na Mjumbe wa Bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba, Mkurugenzi wa Miradi wa DAWASA Mhandisi Lydia Ndibalema.

Wakiwa katika moja ya pampu za kuvuta maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad