HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 23 November 2018

KUPATA MATOKEO NI NJIA NZURI YA KUWANIA UBINGWA- PLUIJM


BAADA ya ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Van De Pluijm amesema kwa timu yake kupata matokeo ni njia nzuri ya kwenda kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ushindi huo unaihakikishia Azam FC nafasi ya kuendelea kubakia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 33 wakiwa  wamecheza mechi 13 bila kupoteza hata huku wakitoa sare michezo 3 na kushinda michezo 10 ya Ligi Kuu.


Pluijm amesema, anaona fahari kubwa sana kwa vijana wake kucheza kwa kujituma na kupata matokeo ambayo anayahitaji hasa kwenye ligi kuu na kielekea kwenye mbio za kuwania ubingwa.


Akizungumzia mechi za ligi kuu, Pluijm amesema  matokeo yao ndani ya Uwanja yanatokana na wachezaji kufuata maelekezo na kujituma ndani ya uwanja.

"wachezaji wangu wanapokuwa uwanjani wanakuwa na uwezo wa kutafuta matokeo kwa juhudi kubwa sana na  hilo ni jambo la kujivunia hasa kwa kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi wanazozicheza,"amesema Pluijm.

"Bado tuna kazi ya kuendelea kutunza rekodi kwa kuwa kuna michezo mingi hasa ukizingatia timu zimeongezeka kwa sasa," alisema.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC izidi kuwa kinara wa ligi ikiwa na pointi 33 wakifuatiwa na Yanga ambao wana pointi 29

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kitapumzika kwa siku tatu kabla ya kuanza mazoezi Jumatatu kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Stand United utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Desemba 4, mwaka huu saa 1.00 usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad