HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 7, 2018

WAHITIMU WA MAFUNZO YA RDP YA TBL WATUNUKIWA VYETI

 Mkurugenzi wa ukuzaji wa Masoko wa ABIn Bev,Kanda ya Afrika Mashariki, Carlos Bernitt,akiongea wakati wa hafla ya kutunuka vyeti wahitimu wa mafunzo hayo. Meneja Masoko na Ukuzaji Biashara wa TBL,Edith Bebwa, akiongea wakati wa hafla ya kutunuka vyeti wahitimu wa mafunzo hayo.
Baadhi wa wahitimu wa mafunzo wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya wahitimu wakionyesha vyeti vyao wakiwa na Maofisa wa TBL na ABIn Bev.
---
Washiriki wapatao 167 wanaofanya biashara kwa kushirikiana na kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) walioshiriki mafunzo ya ujasiriamali na mbinu za biashara yanayojulikana kama Retail Development Programme (RDP) wametunukiwa vyeti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Wanufaika wa mafunzo haya ambao wengi wao ni wamiliki wa mabaa,mameneja wa baa na wafanyakazi wametokea katika wilaya za Temeke, Kinondoni, Kigamboni, Ilala Ubungo na yaliendeshwa na TBL chini ya kampuni mama ya ABIn Bev.

Mkurugenzi wa ukuzaji wa Masoko wa ABIn Bev,Kanda ya Afrika Mashariki, Carlos Bernitt,aliwapongeza wahitimu wa mafunzo hayo “Nawapongeza kwa kuhitimu mafunzo haya na nina imani mkitumia vizuri maarifa mliyoyapata yatawasaidia kukuza biashara zenu na kuleta maendeleo ya kwenu binafsi na jamii nzima kwa ujumla”,alisema Bernitt.

Akiongea kuhusu mafunzo hayo,Meneja Masoko na Ukuzaji Biashara wa TBL,Edith Bebwa,alisema mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa chini ya mpango unaojulikana kama Retail Development Programme (RDP), yanalenga kuwapatia mbinu za kufanya biashara kwa ufasaha wafanyabiashara wadogo wanaoshirikiana nao kibiashara ili kuwasaidia kukua kibiashara.

“Mafunzo haya yameendeshwa na wataalamu wa masuala ya ujasiriamali na washiriki wamewezeshwa kujifunza mambo mbalimbali ya biashara ikiwemo urasimishaji biashara zao,tunaamini yatawasaidia kufanya vizuri sambamba na malengo yetu yaliyokusudiwa”.Alisema Bebwa.

Akiongea kwa niaba ya washiriki wa mafunzo haya,Damas Asenga,alisema kuwa mafunzo haya yamewasaidia kujua masuala mbalimbali ya kuendesha biashara hasa za kuuza vinywaji kama vile utunzaji wa hesabu,mbinu za kuongeza mauzo,huduma kwa wateja,nidhamu ya matumizi ya pesa,jinsi ya kukabiliana na ushindani wa kibiashara na umuhimu wa kufuata kanuni za biashara zilizowekwa na serikali. “Mafunzo haya ni mazuri na tunaiomba TBL iangalie uwezekano wa kuyafikisha kwa wajasiriamali wengi zaidi nchini kote “,alisema Asenga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad