HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 30, 2018

WAHITIMU WA CHUO CHA USTAWI WA JAMII WAMETAKIWA KUTUMIA ELIMU NA UJUZI KUSAIDIA JAMII.

TAASISI  ya ustawi wa jamii (SOCIAL WORK) imewatunuku vyeti wahitimu 1387 katika mahafali ya (42) ya chuo hicho katika ngazi ya astashahada,stashahada, katika fani ya Kazi za jamii kwa Watoto na vijana,Mahusiano kazini na Menejimenti ya sekta ya Umma( industrial Relations and Public Management).

Akizungumzana na wanahabari jijini Dar es salaam katika mahafali hayo
Katibu Mkuu idara kuu ya Maendeleo ya Jamii -Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr.John Jingu amesema kuwa wahitimu wote wamekula kiapo kwa ajili ya kutumikia Taifa na ujuzi waliopatiwa ni rasilimali kwa ajili ya ujenzi wa Taifa kwa ujumla.

"Fani ya ustawi wa jamii( SOCIAL WORK) ni fani nyeti na muhimu katika jamii na wanapaswa kuwa katika sekta mbalimbali kwani wahitimu hawa wamefundishwa kujiajiri na kuajiri watu katika  kaza"amesema Dkt Jingu.

Jingu ameongezea kuwa "alikadhalika katika nchi zilizoendelea kuna hitajika kuwa na mahafisa wa ustawi wa jamii na chuo kwa sasa kinatakiwa kuweka wigo mpana kwa ajili ya kuendelea kuzalisha wataalam kwa lengo la kusaidia jamii na manufaa ya nchi kwa ujumla"

Akizungumza na wanahabari Kaimu Mkuu wa  Taasisi, Mipango,fedha na utawala wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Saliel Kanza, ameeleza kuwa taasisi hiyo  ina changamoto  katika kutekeleza majukumu yake makuu matatu ambayo ni mafunzo,utafiti na kutoa ushauri wa weledi.

"Changamoto hizo ni upungufu wa vifaa vya  Tehama katika kufundishia na kujifunza, uchakavu na upungufu wa Miundombinu ya kujifunza na kufundishia ikiwemo ofisi za walimu,vyumba vya semina,vyumba vya mihadhara(lecture theatre) na zahanati"amesema Kanza.

Pia Kanza amesema pamoja na ufinyu wa Mapato,Taasisi imeendelea kuweka mikakati mbalimbali yakuboresha mazingira bora ya kusomea kwa kubadilisha Matumizi kwa baadhi ya Majengo na kuwa vyumba vya mihadhara.

Aidha amesema  ununuzi wa samani za ofisini na kompyuta ili ziweze kusaidia Wanafunzi na wahadhiri katika kujifunza na kufundishia,Kufanya ukarabati wa Miundombinu ya Taasisi kama vile vyumba vya mihadhara kulingana na uwezo wa kifedha uliopo.

Hata hivyo,mbali na kufanya hayo bado Taasisi Haina uwezo wa kutosha kifedha ili kutatua changamoto tajwa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ,Bi Sophia Simba amewapongeza wahitimu hao na kuwataka watumie elimu yao na ujuzi ili kusaidia jamii katika usuluhishi wa Migogoro mbalimbali katika jamii zetu.

Simba amewahusia wahitimu katika fani zote kuwa ni kila nyanja katika jamii inauhitaji wa Afisa ustawi kwani ni watu wenye ufanisi mkubwa sana katika kutatua matatizo ya jamii,kusuluhisha,kusaidia maeneo yote kwa walemavu,makazini hata Mashuleni.

"wataalam hao ni matumaini ya nchi kuwa watatumiwa vema na Serikali na wadau katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya jamii" amesema Sophia Simba.
Katibu mkuu wizara ya Afya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Dkt John Jingu, akifanya zoezi la  kutoa vyeti kwa wahitimu mbalimbali wa chuo cha Ustawi wa Jamii leo Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa chuo cha Ustawi wa jamii waliotunukiwa tuzo ya uzamili na Dkt John Jingu wakati wa mahafali hayo leo Jijini Dar es Salaam

Wahitimu wa shahada mbali mbali wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakila kiapo wakati wa shughuli ya mahafali hayo mbele ya Mgeni Rasmi Katibu mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt John Jingu  leo Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wahitimu wa shahada mbali mbali katika sherehe za mahafali ya 42 ya chuo cha Ustawi wa Jamii leo Jijini  Dar es Salaam

           

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad