HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 27 November 2018

VODACOM TANZANIA FOUNDATION NA DORIS MOLLEL FOUNDATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA KUSAIDIA WATOTO NJITI HOSPITALI YA NYARUGUSU, KIGOMA

 Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguha (wa tatu kushoto) akipeana mkono na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu (kushoto) wakati wa kupokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba maalumu kwa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) vilivyotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi Doris Mollel kwa wadi ya Hospitali inayohudumia kambi wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel na katikati ni Afisa Msimamizi wa Kambi hiyo, Francis Chokola.
Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguha (wa tatu kulia) akizungumza wakati akitoa shukrani kwa Taasisi za Vodacom Tanzania na Taasisi Doris Mollel kwa msaada walioutoa kwenye hospitali hiyo.
Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguh, akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel wakimjulia hali mama aliyejifungua mtoto Njiti katika Hospitali inayohudumia kambi wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma hivi karibuni, ambapo pia walimzawadia khanga kama sehemu ya faraja kwake.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad