HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 27, 2018

AZAM WAANZA KUJIFUA KUSAKA ALAMA TATU KWA STAND UNITED


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha Klabu ya  Azam FC, kimeanza rasmi mazoezi yale leo  tayari kuanza safari ya kuzisaka pointi kuelekea mchezo ujao dhidi ya Stand United.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Desemba 4 mwaka huu, ambapo Azam FC iko kwenye mwenendo mzuri baada ya kushinda mechi saba mfululizo za ligi hiyo.

Wachezaji wote wa Azam FC wameripoti mazoezini wakiwa na hali nzuri kabisa isipokuwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, ambaye ni mgonjwa.

Beki wa kulia Nickolas Wadada, aliyekuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda, naye amesharejea kundini akiwa ni miongoni mwa wachezaji walioripoti kwenye mazoezi hayo.

Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuendelea na mazoezi kwa wiki hii yote, na siku ya Jumamosi wanatajia  kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya vijana ya timu hiyo (Azam U-20) kwa ajili ya kujiweka sawa utakaopigwa asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex..

Azam FC inayonolewa na Kocha Mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiana na Juma Mwambusi hadi sasa imeshacheza mechi 13 za ligi, ikiwa imesdhinda mara 10 na kutoka sare mara tatu ikijikusanyia jumla ya pointi 33 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifuatiwa na Yanga wenye alama 32 tayari kwakicheza michezo 12 wakishinda 10 wakitoka sare mara 2.

Na katika dirisha la Usajili lililofunguliwa Novemba 15, Azam wameshafanikiwa kunasa saini ya Mshamuliaji wa Kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa huku ikiwaotoa wachezaj wake Ditram Nchimbi, Mbaraka Yusuf kutolewa kwa mkopo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad