HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 22 November 2018

USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA

Na Karama Kenyunko Blogu ya Jamii.
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili, washtakiwa Harbinder Sethi  na James Rugemarila umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa,   washtakiwa wameshindwa kufikishwa mahakamani hapo kwa sababu ya kuwepo kwa shida ya usafiri. 

Wakili wa serikali Emmanuel Nitume ameeleza  hayo Leo Novemba 22,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

"Mheshimiwa, kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na pia washtakiwa wote wanaokabiliwa na kesi hiyo hawapo kwa sababu kuna shida ya usafiri." Amesema Nitume.

Wakati wakili huyo wa serikali akieleza hayo, afisa mmoja wa Magereza aliyekuwemo mahakamani humo aliongeza kuiambia mahakama kuwa washtakiwa hawajaletwa kwa sababu kuna shida ya magari.

Kufuatia melezo hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi  Desemba 6, mwaka huu.

Katika kesi hiyo,Washtakiwa Sethi na Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kusababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad