HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 22 November 2018

Coppa Italia ndani ya StarTimes kuanzia Disemba

Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza ujio wa ligi ya Coppa Italia katika king’amuzi chake kuanzia tarehe 4 Disemba mwaka huu. Ligi hiyo itakuwa ikionekana kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee. Taarifa hiyo imetolewa na Idara ya Mawasiliano ya kampuni hiyo siku ya Jumatano.
StarTimes wamepata haki za kuonyesha michuano hiyo kwa Miaka mitatu yaani kuanzia msimu huu hadi ule wa 2020/21 na itakuwa ikipatikana katika lugha mbalimbali ikiwemo lugha adhimu ya Kiswahili.

Coppa Italia ni moja kati ya michuano yenye ushindani wa hali ya juu na msisimko wa aina yake barani Ulaya kwani huzikutanisha timu 16 zinazocheza katika ligi kuu ya nchini Italia maarufu kama Serie A, daraja la kwanza Serie B na Serie C ili katika mzunguko wa kwanza kutafuta timu 8 ambazo zitaungana na timu 8 za juu katika msimamo wa ligi kuu (Serie A) ili kucheza hatua ya 16 bora.

“Mpira wa kiitalia ni moja ya soka zinazovutia sana kutazama ndio maana tumewaletea wateja wetu kandanda hili la kusisimua. Pia ni katika mwendelezo wetu wa kuhakikisha hatuishiwi soka hata pale wengine wanapokaukiwa. Pia Italia kuna timu nyingi na bora ambazo zitashiriki katka Coppa Italia, Mfano Juventus, timu za jiji Milan, Napoli na AS Roma ambazo zitashiriki”. Sam Gisayi, Afisa Mahusiano wa StarTimes.

“Kwa hiyo wateja wetu wanao uhakika wa kumtazama Cristiano Ronaldo, Edin Dzeko, Gonzalo Higuain, Paulo Dybala na sasa kuna tetesi msweden Ibrahimovich atarejea kwenye klabu ya AC Milan hivyo burudani itaongezeka maradufu”. Aliongeza

Mbali na Coppa Italia, mwezi Disemba StarTimes watakuwa na michuano ya Club World Cup ambayo kwa kuanzia tarehe 12 kupitia chaneli zao za michezo. Kwa mara nyingine tena wateja wake wana nafasi ya kuwashuhudia Mabingwa Real Madrid wakijaribu kutetea taji lao, ila mara hii watahijati kufanya hivyo bila Cristiano Ronaldo.

StarTimes pia wanaendelea kuonyesha ligi ya Bundesliga pamoja na ile ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, na wiki ijayo kutakuwa na raundi nyingine ya EUROPA ligi ambayo nayo huonyeshwa kupitia StarTimes Pekee katika chaneli zao za michezo. Na wateja hutakiwa kulipia aidha kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 14,000/= tu au SMART kwa Tsh 21,000/= pekee.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad