HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 9, 2018

UPELELEZI KESI YA KITILYA NA WENZAKE BADO HAUJAKAMILIKA

Na Karama Kenyunko blogu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa na upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili,  aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kuwa wanawasiliana na wachunguzi ili wajue upelelezi umefikia wapi.

Mbali na Kitilya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni inayoshughulikia  Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma), washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa benki ya Stanbic, Sioi Solomon.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Novemba 9.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi dhidi ya washtakiwa hao ilipoletwa kwa ajili ya kutajwa. Wakili Mwita amedai upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, bado wanaendelea kuwasiliana na wachunguzi.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 16, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.
Washitakiwa wote kwa pamoja  wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550   kwa  Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.

Wanadaiwa kuwa  Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita , wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo  na zililipwa kupitia  Kampuni ya Egma T Ltd.

Washitakiwa  hao wanadaiwa kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani milioni sita katika akaunti tofauti tofauti  za benki.

Kati ya  Machi 2013 na Septemba 2015, wanadaiwa  kuwa waliweka pesa hizo katika akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na kampuni ya Egma na kwamba walipaswa kufahamu kuwa pesa hizo ni mazao ya uhalifu wa kughushi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad