HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 9 November 2018

STARTIMES TANZANIA WEKEZENI KATIKA SEKTA YA FILAMU ILI KUPATA KAZI BORA NA ZITAKAZOTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA- TFB

Na Mwandishi Wetu.
Bodi ya Filamu imeitaka Startimes kuwekeza katika ya Filamu na Uigizaji nchini ili wapate kazi bora na zitakazotumia teknolojia ya kisasa badala ya hali ya sasa ambapo wanaonufaika ni madali kupitia kazi ambazo zimetengenezwa na Wadau wetu bila kuwa na manufaa ya kutosha.

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo katika ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam alipokutana na maofisa wa Kampuni hiyo kujadili ushirikishwaji wa Wanatasnia wa Filamu na Michezo ya Kuigiza kwenye kazi zinazoratibiwa na kampuni hiyo ikiwemo Filamu, Uigizaji na Matangazo.

“China ni kati ya nchi ambazo zinatumia teknlojia ya kisasa katika uzalishaji wa Filamu hivyo wekeni mkakati wa muda mfupi wa agalau kupeleka vijana na wanasekta ya Filamu kama waigizaji, watayarishaji, wapiga picha, waongozaji na waandishi wa miswada wakaongeze taaluma katika kampuni za uzalishaji nchini China ili hizi kazi zinazozalishwa ziwe katika ubora unaoendana na teknolojia ya kisasa; Alisema Fissoo.

Aliongeza kuwa umefika wakati wa kazi za Tanzania pia kuwekewa lugha ya kichina ili ziingie katika soko la China kama ilivyo kwa kazi za kichina zinazowekewa sauti ya Kiswahili. Zipo kazi nzuri za Watanzania zinanunuliwa lakini hazitiwi sauti lakini pia hazinunuliwi kwa wenye kazi wenyewe hivyo ni lazima tusimamie Sheria, Kanuni na Taratibu ili pande zote mbili ziweze kunufaika

“Tunahitaji ulinzi wa mikataba kwa wadau wetu hatuko tayari kuona makampuni yanawatumia wanatasnia wa filamu na uigizaji kujipatia faida wao pasipo kuwanufaisha wadau wetu wao moja kwa moja” Alisema Fissoo.

Kwaupande wa Startimes Tanzania kupitia kwa Meneja Masoko Bi. Zamaradi Nzowa ambaye aliambatana na wanasheria wawili aliishukuru Bodi ya Filamu (TFB) kwa muongozo na ushauri sahihi wa namna ya kuendeleza Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kupitia uwekezaji ambapo alimuahidi Katibu Mtendaji kuanza mchakato wa kuwawezesha waandaaji wa Filamu nchini kupitia mafunzo ya maeneo mbalimbali katika utengenezaji na uigizaji wa Filamu.

“Startimes iko tayari kuhakikisha inachangia maendeleo ya Tasnia ya Filamu nchini kwa kufanya uwekezaji utakaokuwa chachu ya Tasnia nzima na Taifa kwa ujumla kwasababu teknolojia ya Tasnia ya Filamu inazidi kukua na inahitaji weledi na utaalamu wa hali ya juu hivyo tutajitahidi kuhakikisha tunawekeza kwenye Tasnia hii ili kupata kazi zenye ubora na zitakazo kuwa na ushindani kimataifa”

Uwekezaji katika Tasnia ya Filamu utasaidia kulinda na kukuza tamaduni zetu kwa kuwa na uzalishaji unaotumia teknolojia ya kisasa hivyo itapelekea kukuza soko la Filamu za kitanzania ndani na nje nchi.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo akimuga Meneja Masoko wa Startimes Tanzania Bi. Zamaradi Nzowa, mara baada ya kumaliza kikao kwenye ofisiza Bodi hiyo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
: Maofisa wa kampuni ya Startimes leo walipokuwa kwenye kikao kuhusu Wadau wa Filamu na Michezo ya kuigiza nchini katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko Bi. Zamaradi Nzowa, Katikati ni Mwanasheria Abdul Mbeo na Mwanasheri Justine Ndege.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad