HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 14, 2018

STARTMIMES YAJA NA LIPA TUKUBUSTI MSIMU WA KRISMASI


KUELEKEA msimu wa Krismasi kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya Startimes imekuja na promosheni kabambe kabisa Kwa wateja wao pendwa na kuwashauri  wale ambao bado hawajajiunga na familia ya StarTimes kuwa msimu huu wa siku kuu wanaletea ‘LIPA TUKUBUSTI’ambayo inawapatia faida nne Katika kila atakachonunua kutoka kwao ambapo kama kampuni  watawabusti au kuwaongezea wateja zaidi.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Terrace, Slipway Masaki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waigizaji maarufu wa Bongo Movie pamoja na wasanii wa Muziki wa kizazi Kipya.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja masoko wa Startimes Davis Malisa amesema kuwa Promosheni ya LIPA TUKUBUSTI kwa wateja wa StarTimes itawapa vifurushi vikubwa zaidi kila watakapolipia na kujiunga na vifurushi vyao vya kawaida kwa malipo ya mwezi Mzima. Hali kadhalika kwa wateja wapya watapatiwa Antena bure kila watakaponunua king’amuzi cha Antenna kwenye maduka na mawakala wa StarTimes.

“Vifurushi vyetu, kwa wateja wa Antenna Ukilipia kifurushi cha NYOTA kwa Tsh 8,000/= utapata kifurushi cha MAMBO kwa mwezi mzima, Ukilipia kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 14,000/= tutakubusti hadi kifurushi cha Uhuru kwa mwezi mzima, na ukilipia Uhuru utapatiwa wiki moja bure" Ameeleza Malisa.

Aidha Malisa amesema kuwa
 kupitia promosheni hiyo wateja watanufaika kwa Kupata dishi bure kila watakaponunua luninga za Kidigitali za StarTimes za ukubwa wowote ule kuanzia Inchi 24, 32, 43 hadi ile Luninga Smati ya Inchi 55.

Kwa upande wa maudhui, Msimu huu wa Sikukuu StarTimes wamejipanga kuleta burudani hasa  Filamu Mpya kabisa za Bongo Movie Huku shindano la Bongo Star Search likiendelea, na kufikia hatua ya mchujo ndani ya Studio na shindano hilo linaendelea kuonekana Kila siku saa tatu Usiku kupitia chaneli ya StarTimes Swahili Pekee.

Kwa upande wake meneja maudhui wa Startimes Zamaradi Nzowa amesema kuwa, "Tuna furaha kubwa kuwaletea filamu za Bongo Movie Mpya kabisa kwa mwezi mzima wa Disemba, filamu ambazo zina mastaa tunawaowapenda na kuwafatilia kila siku. Ni wakati wa kutengeneza kumbukukumbu nzuri na wale tuwapendao na StarTimes inalifanikisha hilo. Sio hayo tu bali tunaleta Msimu mpya wa Coppa Italia kwa mara ya kwanza kupitia StarTimes pekee, utamshuhudia Cristiano Ronaldo na Juventus kuanzia Disemba 5 kupitia chaneli zetu za Michezo”. Ameeleza Zamaradi.

Pia Zamaradi amesema kuwa,   "Ligi ya Bundesliga inayoonyeshwa na StarTimes pekee, inaendelea sambamba na ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, huku zikichagizwa na Ligi ya EUROPA. Bila kusahau chaneli na vipindi vya watoto kama Jim Jam, POP na chaneli mpya ya ST Kids ambavyo vitahakikisha watoto wako wanakuwa na siku kuu ya kipekee.
Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao pendwa kwenye msimu huu wa Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
 Meneja Maudhui wa Startimes Zamaradi Nzowa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa tasnia ya Filamu pamoja na muziki wa kuhusu maudhui zitakazopatikana kwenye vifurushi vya Startimes wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao pendwa kwenye msimu huu wa Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen akizungumza kuhusu Startimes wanavyoshirikiana kwenye kuibua vipaji vya wasanii wachanga wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao pendwa kwenye msimu huu wa Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad