HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 15, 2018

Mradi mkubwa wa kunoa bongo za ufundistadi wazinduliwa

 Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO, Faith Shayo (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika. Kushoto ni Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem.
 Kutoka kushoto ni Mratibu wa mradi wa BEAR ll, kutoka makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Whan Sik Kim, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde, Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song pamoja na Mratibu wa mradi wa BEAR II kutoka ofisi za Unesco Nairobi, Bw.Teeluck Bhuwanee wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo akitoa neno la ukaribisho wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde akizungumza kwa niaba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song akitoa salamu za serikali ya Korea Kusini wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mratibu wa mradi wa BEAR II kutoka ofisi za Unesco Nairobi, Bw.Teeluck Bhuwanee akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa UNESCO ukanda wa Afrika Mashariki, Anne Therese Ndong Jatta Kusini wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mratibu wa mradi wa BEAR ll, kutoka makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Whan Sik Kim, akiwasilisha mkakati wa taasisi hiyo kuhusu ufundi stadi na maana yake katika mradi wa Bear ll nchini Tanzania wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Wasilisho hilo lilikuwa ni pamoja na matokeo ya utafiti.
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo akitoa neno la shukrani kwa serikali ya Korea ya Kusini kupitia Shirika la KOICA kwa ufadhili wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.\
Injinia Enock Kayani kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia akizungumzia mradi na matokeo yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mkurugenzi Mtendaji Mamalaka ya Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Bw. Bakari Silima akitoa wasilisho kuhusu mradi unavyoweza kutekelezwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.

 Sehemu ya wadau kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA pamoja wadau wa maendeleo walioshiriki uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Washiriki kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA pamoja wadau wa maendeleo wakijadili mwongozo kuhusu makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa BEAR II kwenye vikundi kazi wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Mgeni rasmi pamoja na washiriki wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.

Na Mwandishi wetu
MRADI mkubwa wa kufunza walimu wa wasimamizi wa mafunzo ya ufundi standi umezinduliwa kwa kufanyika kwa warsha itakayosaidia kutoa mwelekeo wa mradi .
Akizungumza katika warsha ya mradi huo wa BEAR ll unaofanyika katika nchi tano zikiwamo Tanzania na Uganda katika awamu yake ya pili, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Noel Mbonde akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo alishukuru serikali ya Korea na UNESCO kwa kusaidia kupatikana kwa elimu hiyo nchini.
Nchi zingine ni Ethiopia, Kenya, Madagascar, Tanzania na Uganda.
Alisema elimu hiyo itasaidia kuboresha na kuleta uwiano kati ya mafunzo ya ufundi stadi na matumizi yake katika viwanda nchini.
Alisema kuna malalamiko kwamba wahitimu wanashindwa kwenda sanjari na matakwa ya shughuli zao katika viwanda hivyo mradi huo ni msaada mkubwa.
Mradi huo wenye changio la dola za Marekani milioni 1.56 kwa kipindi cha miaka mitatu zinatarajiwa kusambazwa kwa mamlaka mbalimbali za mafunzo nchini yakiwemo mafunzo ya ufundi stadi zitakazowezesha wafundishaji kutoa mwanga unaotakiwa kwa mafundi stadi. Mamlaka hizo ni pamoja na TCU, Baraza la Ithibati (NACTE) nakadhalika.
Alisema mradi huo anaamini utatafuta tatizo la kutoa mafunzo kwa walimu wa ufundi na kuoanisha mahitaji ya viwanda.
Alisema ingawa awamu ya kwanza haikufika nchini Tanzania, awamu hii ya pili iliyoletwa nchini kwa miaka mitatu ina msaada mkubwa kwa watanzania ambao wanajiandaa kuwa nchi ya viwanda.
Pamoja na kushukuriwa, Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song amesema taifa lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba linawezesha elimu ambayo ni msingi mkubwa wa maendeleo.
Alisema kwamba nchi yake ipo tayari kusaidia Tanzania katika elimu na kilimo kupitia Shirika lake la KOICA.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO, Faith Shayo alisema kwamba lengo kubwa la mradi huo ni kuboresha mafunzo ya ufundi nchini.
Pamoja na maboresho pia lengo lilikuwa kuweka njia inayouwiana na masomo hayo ili kuhakikisha kwamba yanachangia katika ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.
Mratibu wa mradi wa BEAR II, Bw.Teeluck Bhuwanee alisema ni matumaini yake kwamba ushirikiano kati ya serikali, Korea Kusini na Unesco utasaidia kuboresha elimu ya ufundi nchini.
Kuzinduliwa kwa BEAR II kunaashiria utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kuendeleza utaalamu (NSDS)  kuanzia mwaka 2016/17 hadi 2025/26 wenye lengo la kuwa na wafanyakazi wataalamu na wenye ushindani.
Katika warsha hiyo Wizara ya Elimu Sayansi na Elimu ya Juu imesema kwamba itahakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa na kuwataka wadau wote kushiriki katika kuufanikisha .
Aliwataka kila mdau kuikumbatia dira mpya ya utendaji inayobuniwa na kufikiriwa katika Bear ll kwa lengo la kuimarisha uchumi.
Bw. Teeluck Bhuwanee, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa UNESCO ukanda wa Afrika Mashariki, Anne Therese Ndong Jatta, alisema kwamba kuna kazi kubwa inayotakiwa kufanywa ili kuvikokoa viwanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad