Kwa wapenzi wa soka kote duniani hakuna raha kama kuona timu mbili kubwa zikivaana Uso kwa Uso tena zikiwa na mashabiki lukuki. Miongoni mwa mechi za kusisimua sana katika Ulimwengu wa soka ni ile ya watani wa jadi wawili nchini Ujerumani, ni miamba wa jiji la Dortmund na wababe wa jiji la Munich. Borussia Dortmund vs Bayern Munich na Der Klassiker ndio jina halali la mchezo huo.
Dortmund ambao wanaongoza ligi watakuwa nyumbani katika dimba la Signal Iduna Park Jumamosi hii tar 10, majira ya 2:30 saa za Afrika Mashariki, kuwakabili mabingwa wa ligi hiyo msimu uliopita Bayern Munich.
Mpaka sasa Dortmund hawajapoteza mchezo wowote katika Bundesliga msimu huu huku Bayern wao wakiwa wameshapoteza michezo miwili hadi sasa. Pia Dortmund waliambulia vipigo katika mechi tatu zilizopita za Der Klassiker, lakini wikendi hii wanayo nafasi ya kubadilisha bahati yao kwani wanacheza kandanda safi msimu huu huku wapinzani wakionesha kutowepo katika kiwango kilichozoeleka kwa miaka kadhaa sasa.
Kwa wapenzi wa Soka hapa nchini mchezo huu utakuwa MUBASHARA kupitia chaneli ya ST World Football ndani ya king’amuzi cha StarTimes ambao ndio warushaji pekee wa ligi hiyo yenye kasi zaidi barani Ulaya.
Kuchagiza burudani hiyo mtazamaji ana nafasi ya kuchagua kupata uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi cha StarTimes kwenye luninga yake ili kuongeza umakini wa ufatiliaji wa mchezo huo.
Ligi ya Bundesliga inapatikana kwa urahisi sana ambapo mteja wa StarTimes atatakiwa kulipia kifurushi cha MAMBO kama anatumia kisimbuzi cha Antenna kwa Tsh 14,000 tu, na kwa watumiaji wa Visimbuzi vya Dish ni kifurushi cha SMART ambacho kinapatikana kwa Tsh 21,000 tu.
Mbali na ligi ya Bundesliga, StarTimes wanaonyesha ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, UEFA EUROPA league na Coppa Italia ambazo hupatikana katika chaneli zao za michezo kwa kiwango cha HD (High Definiton).
No comments:
Post a Comment