HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 22, 2018

MOI YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA WA KUONDOA UVIMBE KWENYE MISHIPA YA DAMU YA UBONGO

NA KHAMISI MUSSA
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imefanikiwa kufanya upasuaji kwa mara ya kwanza hapa nchini kuondoa vivimbe katika mishipa ya damu ya ubongo (Aneurysm) ya mgonjwa. Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Alhaji Dkt. Hamisi Shabani.(pichani) amesema kwamba kabla ya hapo wagonjwa walikuwa wanafanyiwa upasuaji huo nje ya nchi kwa gharama kubwa isiyopungua shilingi za kitanzania milioni 100.

Akiongea na waandishi wa habari, Dkt.Shabani amesema kwamba aina hii ya upasuaji unahitaji darubini na vifaa tiba maalum ili kufanikisha upasuaji huo. "Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutupatia vifaa vyote ambavyo ni muhimu ili kufanikisha upasuaji huu.Na kuanzia sasa wagonjwa kama hao hawatapelekwa tena nje ya nchi watafanyiwa hapa nchini kwa gharama nafuu isiyozidi shilingi milioni 10".Naye Angel Msangi (37) ambaye ni mgonjwa wa kwanza kufanyiwa aina hii ya upasuaji alisema kwamba anamshukuru Mungu kwa kufanikiwa kuwa mgonjwa wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa aina hiyo kwa mafanikio kwani asingemudu gharama za upasuaji nje ya nchi.

"Pia nawashukuru Madaktari wa Taasisi ya Mifupa MOI kwa kuniwezesha kunifanyia upasuaji huu na kuwashukuru wauguzi wa Taasisi hii kunifanyia upasuaji huu na sasa nina uhakika wa kuishi kwani nilikuwa nasumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu na nikiweka kitu nakuwa sijui nimekiweka wapi, nikiwa nimekula nasahau kama nimekula, kwa hiyo kwangu ikawa ni shida tayari".

Aidha Dkt. Shabani alisema kwamba aina hii ya vivimbe huwapata watu wengi lakini sio rahisi kugundulika kama una tatizo bila kufanya kipimo maalum cha CT-Scan. " Asilimia 5 ya watua wazima wenye umri kuanzia miaka 30 ndio waathirika wakubwa. Nchini Marekani wamefanya utafiti na kugundua kwamba asilimia 5 ya watu wazima wanaathirika na matatizo haya.Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kwamba kwa kila watu 100 watu 10 wanakabiliwa na tatizo hili". Alisema Dkt Shabani. Athari za vivimbe vya damu kwenye ubongo ni pamoja na kupooza na kupoteza fahamu na kumbukumbu kwa mgonjwa.

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akimuelekeza Angel Msangi kufanya mazoezi ili ajiridhishe mgonjwa wake wakwanza aliye fanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe katika mishipa ya ubongo kujiridhisha kama amepata nafuu apate kumpa ruhusa ambapo upasuaji huo ulichukua muda wa saa 6. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSS)
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sehem ndogo iliyotumika kuondoa uvimbe huo

Angel Msangi akizungumza jambo na waadishi wa habari leo katika Taasisi ya Mifupa MOI, Dar es Salaam. wa pili kulia ni Askari wa jeshi la Polisi CCP Moshi, Julius Msangi ambaye ni mume wa Angel Msangi na wa kwanza kushoto ni Dkt, Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad