HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 5, 2018

MHANDISI NA MGANGA MKUU WILAYA YA MBULU WAKALIA KUTI KAVU

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alitoa amri ya kuwaweka ndani Mganga Mkuu pamoja na Mhandisi  wa ujenzi wa kituo cha Afya Mbulu baada ya kubaini madudu na mapungufu mengi katika ujenzi wa kituo hicho kilichopo kata ya Dongobeshi  Wilayani humo.
 Dkt. Ndugulile alibaini madudu katika kituo hicho cha Afya baada ya kukagua ujenzi eneo la pasuaji na sehemu ya kuifadhi maiti na kugundua makosa ya kiufundi katika ujenzi wa sehemu hizo nakuoji Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Joseph Foma kwanini aliruhusu makosa kitaalamu kutozingatiwa katika hatua za wali za ujenzi .
Aidha Mganga Mkuu wa Wilaya pia alishindwa kuthibitisha ikiwa aliwai kufika katika eneo la ujenzi wa kituo hicho na kukili kuwa alifika siku moja kabla ya Naibu Waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho jambo lilosababisha Naibu Waziri kumwagiza Kamanda Mkuu wa Polisi Wilayani humo kumweka ndani mara moja Mganga Mkuu wa Wilaya.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri pia aliomba kupatiwa ramani ya mchoro wa Kituo hicho kutoka kwa Mhandisi wa ujenzi wa Kituo hicho Mhandisi Samweli Bundala ambaye pia alishindwa kuonesha ramani ya ujenzi pamoja lakini pia kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kunusuru Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo matokeo yake naye ikitolewa amri ya kukamatwa kwake.
‘’Kamanda Mkuu Wilaya weka ndani wote wawili akili iwakae sawa inakuwaje Mhandisi unakaa eneo la ujenzi bila kuwa na ramani ya ujenzi na Mganga Mkuu unashindwa kutoa ushauri kwa wataalamu wa ujenzi kujenga kituo cha Afya bila kuzingatia vigezo vya kitaaluma katika ujenzi wa eneo la upasuaji”. Sehemu ya upasuaji ni sehemu takatifu alikaliliwa akisema Dkt. Ndugulile ambaye kitaaluma ni Dkt. Bingwa wa tiba za binadamu. 
Aidha Dkt. Ndugulile alitaka kujua kiwango cha elimu cha Mganga Mkuu huyo wa Wilaya na kuoji kama alipitia sawasawa masomo ya udaktali kwa alijua pasiposhaka kuwa kwa Dkt. aliyefuzu vyema masomo yake angejeua na kushauri mhandisi wa ujenzi namna bora ya ujenzi wa miundombinu ya hospitali.
Pamoja na makosa katika ujenzi wa maeneo hayo muhimu lakini pia Naibu Waziri Ndugulile alishangaa kuona hata miundombinu ya maji taka ya kituo hicho haikuzingatia matakwa ya namna gani mfumo wa maji ya eneo la upasuaji inavyopaswa kufungwa kwa kuwa Daktari anapokuwa katika eneo hilo la upasuaji usukuma milango kwa kutumia bega moja lakini pia usukuma koki za bomba kwa kiwiko vigezo ambavyo havikuzingatiwa wakati wa ujuenzi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa amebeba mtoto Constantine alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Dareda iliyoko Wilaya ya Babati Vijijini katika ziara yake kuangalia huduma za hospitali na vituo vya Afya Mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad