HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 5, 2018

DKT ABBAS: SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA 67

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Serikali imesema ndani ya miaka mitatu inatarajia kujenga vituo vya afya 67 katika maeneo mbalimbali nchini. 

Aidha imesema ndani ya kipindi hicho upatikanaji wa  dawa kwa wastani kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini umefikia asilimia 90.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas, amesema hayo leo Novemba 3.2018 alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) yaliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Akizungumza katika mafunzo hayo, Dk. Abbas amesema serikali imeahidi kuboresha huduma ya afya mijini na vijinini kwani tangu kupata Uhuru imejenga Hospitali 77 na sasa inaenda kujenga vituo 67 na kuhakikisha azma ya kutekeleza Huduma ya afya inatekekezwa.

Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Dk. Abbas amesema miaka ya nyuma upatikanaji wa dawa kwa zahanati, vituo vya afya na hospitali ilikuwa shida hasa kutokana na mfumo uliokuwa unatumika kusambaza lakini kwa sasa jambo ambalo sasa jambo hilo limedhibitiwa.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Tano imetenga bajeti ya kutosha hali MSD kuweza kuagiza na kusambaza dawa kwa wakati.

"Kwa sasa Tanzania imekuwa kimbilio la nchi zingine kwa kuleta wagonjwa wao kutokana na uwepo wa vifaa tiba na wataalam katika hospitali mbalimbali nchini ambao wanatoa mpaka tiba za kibingwa", amesema Dk. Abbas.

Ameongeza kuwa, Tanzania sasa imeanza  kuwa kimbilio kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa katika hospitali zetu, sasa hivi wanapokelewa wagonjwa kutoka Comorro,  Burundi, Rwanda,  Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na nchi zingine wanakuja Muhimbili kuja kutibiwa. 

Dk Abbas pia ameushukuru mfuko wa NHIF katika miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano kwa kufanya mambo mazuri ikiwemo kusaidia ujenzi wa hospitali na kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia Milioni 17.

Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Mbaruku Magawa  amesema,mkutano huo unalengo la kuweka mikakati ya pamoja baina ya NHIF na waandishi wa habari juu ya kuelimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya.

" Malengo ya kukutana na waandishi wa habari ni kuhimarisha uhusiano na kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha mfuko huo na kusaidia Jamii kutambua umuhimu Wa bima ya afya na faida zake, amesema Magawa.

Ameongeza kuwa, mafanikio yaliyopo katika mfuko huo yametokana na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi na kwa sasa mfuko unafanya jitihada ya kuongeza wigo la wanachama hivi karibuni tutazindua vifurushi vya wanachama vitakavyowawezesha watu wengi kujiunga na bima ya afya kadri ya uwezo wao.

Naye, Katibu Mtendaji wa DCPC,  Hussein Siyovelwa ameishukuru NHIF kwa kukubali kuandaa mafunzo hayo kwa wana DCPC kwani yatasaidia kuongeza kuelewa kwa waandisi wa habari kuhusiana na masuala ya bima ya afya ya NHIF
 Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas  akizungumza na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kuhusiana na mafunzo ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) yalifanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF Mbaruku Magawa akizungumza na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kuhusiana na bidhaa zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)katika mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mtendaji wa DCPC  Hussein Siyovelwa akizungumza kuhusiana umuhimu wa wanachama kufanya kazi kwa ukaribu na NHIF katika utoaji wa taarifa kwa jamii .
 Meneja wa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Angela Mziray akitoa maelezo  kwa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC)  kuhusiana na utoaji wa elimu katika makundi mbalimbali  ya  katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Picha za pamoja za makundi mbalimbali  katika mafunzo( Picha na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad