HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 14 November 2018

MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32

KATIKA  hali  isiyoya kawaida   kikao  cha  baraza la madiwani  wa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa ambacho  kwa wiki  iliyopita  madiwani  wa chama  cha mapinduzi (CCM)  walisusia  kikao   hicho  mstahiki  meya   Alex  Kimbe amewashangaza  wengi  baada ya  kuendesha  kikao  kwa  dakika 32  na  kugoma kusikiliza  hoja binafsi .

Kikao   hicho  kilianza  saa 2.00  hadi saa 2.32  huku  madiwani  takribani 10 wa  chama  cha  demokrasia na maendeleo (Chadema)  wakiwa na ukumbini na CCM   akiwemo  diwani  mmoja pekee  na   naibu  meya  Joseph  Lyata    kiliweza  kuendeshwa  kwa aina  yake  baada ya  mstahiki  meya   kufungua  kikao  hicho  kwa   sala  baada ya hapo kuwaita  bila  kutokea wajumbe  watatu wawili wa CCM na mmoja wa  Chadema  kuuliza maswali ya  papo kwa  papo kwa  meya   .

Kutokana na  wajumbe hao  wa  kikao  kutokuwepo  alifunga  zoezi hilo  na  kuendelea  na agenda  nyingine za  kikao  ikiwa  ni pamoja na  kusoma  taarifa  za  kamati  mbali mbali  na  kuruhusu  wenye  maswali  juu ya kamati hizo  kuuliza maswali  baada ya  hapo  alitangaza  kuzikataa  hoja  binafsi  ambazo   takribani  tatu ambazo  zilikuwepo  kwa madai ya  kutozingatia  kanuni  za  baraza  hilo kwa  hoja  hizo  kufikishwa kwa maandishi kabla ya   kuletwa katika  baraza .

"  Ndugu  wajumbe  kwa  kuwa hakuna  hoja binasi  zilizopo  ni za mdomo  tuu  naomba  kumkaribisha katibu  wa  kikao kwa  maneno  machache na  baada ya  hapo  nifunge  kikao  chetu "  alisema  meya  Kimbe  .

Kuwa  anawashukuru  wajumbe  waliofika kwa  wakati katika  kikao  hicho  ambacho  kimsingi  kilitangazwa  kuanza saa 2 .00 asubuhi   hivyo  wajumbe  waliochelewa  wamechelewa  kikao   hicho  alisema  na  kutangaza  kufunga  kikao  huku  baadhi ya  madiwani  wakiendelea  kuwasili  ukumbini .

Wakizungumza mara  baada ya  kikao  hicho aliyekuwa  meya wa Manispaa ya  Iringa Aman Mwamwindi (CCM)  alisema anashangazwa na hatua ya  kikao  kumalizika kwa  muda  mufupi  wakati  kulikuwa na hoja za  msingi  hasa  kwenye kamati ya mazingira  juu ya  eneo la Kihesa  Kilolo  eneo la  uwekezaji  ambalo waziri  wa  ardhi nyumba na maendeleo ya makazi na  waziri wa TAMISEMI  walishauri  eneo hilo  kutojengwa  viwanja  vya   michezo na badala  yake  kujenga vitega uchumi kama  ukumbi wa  mikutano wa AICC .

lla alisema anashangazwa  kuona anapingwa na meya  na  kuwa   hoja   hiyo  haina nafasi katika  kikao  hicho  na  badala yake  kuzuia  kujadiliwa na  kukimbilia  kufunga  kikao .

 Diwani  wa kata ya  Mivinjeni  Frank  Nyalusi (Chadema)  alisema anampongeza  mstahiki meya kwa  kuendesha  vikao  kisasa na  kuzingatia  muda  wa  kikao kwani  alisema   hoja  nyingi  zilizotolewa  tayari  zilijadiliwa katika  kamati mbali mbali  hivyo baraza la madiwani kazi yake  ilikuwa ni  kupitisha  taarifa  za kamati .

Hivyo  alisema  muda  mfupi  wa  uendeshaji wa  kikao  hicho  ni  sawa  na  waliochelewa  yawezekana  wamefanya hivyo kwa malengo yao  lakini kikao   hicho  kwa  kuwa ni kikao cha  pili kuitishwa  baada ya madiwani wa CCM kususia kikao  kilichopita  baraza  hilo  lingeweza kuendeshwa  hata kama  ukumbini kungekuwa na diwani  mmoja.

Kwa  upande wake  diwani wa kata ya  Mwangata  Edward  Nguvu (CCM)  akielezea  kuhusu  kuhakakishwa  kwa  kikao  hicho  alisema  pamoja na kuwa  yeye ni mgeni  katika baraza  hilo akiwa na  miezi miwili  toka  achaguliwe  ila  ameshangazwa na kikao  nyeti kama hicho kutumia  muda  mfupi  hivyo .

Kwani  alisema  kikao  cha baraza la madiwani ni kikao  ambacho kinajadili mambo ya maendeleo ya  kata na  Halmashauri kwa  kina  zaidi hivyo  hakukuwa na  sababu ya  kuharakisha  kikao  hicho  kwani  pamoja na kuwa  alifika dakika  za  mwisho  kwenye  kablasha  walilopewa  kulikuwa na makosa  mengi  ambayo  yangefanyiwa  usahihisho  pia  wangetumia  muda  huo  kujadili mambo  mengi  zaidi.

Nguvu  alisema  yawezekana  meya  aliendesha  kikao  hicho kwa  hofu  kuwa  huenda  madiwani wa  CCM  wangekuja na  hoja  asiyoipenda  ya  kumkataa ama  vinginevyo  .

Naibu  meya  wa Manispaa ya  Iringa  Joseph  Lyata  alisema muda  wa  kuanza  kikao kila  diwani  alikuwa anaujua na  kuwa kumalizika kikao mapema  sio  tatizo  ila  tatizo kama  kungekuwa na jambo  ambalo halijafanyika .
Baadhi ya madiwani  Halmashauri ya  Iringa  wakiwa katika  baraza leo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad