HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 14, 2018

MADIWANI TABORA WATAKA OCD KWENDA KUJIBU TUHUMA ZA MGAMBO KUPIA WANANCHI

Na Tiganya Vincent, Tabora
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora limetaka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora aitwe kwa ajili ya kujibu tuhuma zinawakabili baadhi ya askari wake na migambo za kuwapiga na kuwaibia wananchi mali zao wakati wa Doria zao.

Madiwani hao wametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha robo ya kwanza ya Baraza hilo kufutia hoja iliyowasilishwa na Diwani wa Kata ya Itojanda Alphonce Shushi ya uwepo wa vitendo vya unyanyasaji wananchi vinavyofanywa na Mgambo.

Alisema Migambo hao kwa kushirikiana na baadhi ya Askari wanapokuwa katika Doria wamekuwa wakiwapiga na kuwanyanyasa na kuwahumiza baadhi ya watu.

Aliongeza kuwa baadhi yao wamekuwa wakidiriki hata kuchukua mali za watu wanapowakata kwa kisingizio cha kufanya Doria.

Naye Diwani wa Kata ya Isevya Ramadhani Shabani alisema migambo hao badala ya kusaidia kupambana na uhalifu wao ndio wako mstari wa mbele kuiba na kuwanyanyasa wananchi mitaani.

Alisema kuwa kazi yao kubwa ni kupiga watu na kufukizana na madreva wa pikipiki na wakati mwingine kuwabambikizia makosa.

Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Ifucha Rose Kilimba alihoji sababu zilizomfanya OCD kushindwa kuhudhuria kikao  Baraza la Madiwani wakati siku zote amekuwa akihudhuria au akituma mwalilishi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti siku zote OCD anahudhuria vikao leo kwanini ameshinwa kuhudhuria na hata kumtuma mwalilishi labda amejua kuwa tutamuuliza juu ya unyanyasaji unaofanywa na hao migambo anawatumia” alisema.

Alisema kitendo hicho kinasikitisha kwa walitaka wamweleze kero ambazo Migambo hao kwa kushirikiana na baadhi ya askari wanasababisha.

elezea kusikitishwa kwake na kitendo cha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora kushindwa kuhudhuria kikao chao licha ya kumpatia taarifa kwa ajili ya kujibu tuhuma zinawakabili baadhi ya askari wake na migambo.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Ng’ambo George Mpepo alimuomba Mstahiki Meya kusogeza mbele hoja hiyo ili OCD apewe taarifa ya kuhudhuria kwa ajili maoani na maswali ya Madiwani kuhusu  kero ambazo wanazipata wananchi kutoka na askari na migambo wanapokuwa katika Doria.

Alisema baadhi ya Migambo hao wanahistoria ya wizi na hivyo wanatumia fursa hiyo na Doria kuchukua mali za wananchi.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora. Leopold Ulaya amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wake kuhakikisha anamweleza Mkuu huyo wa Polisi aweze kuhudhuria kikao kijacho(kesho) kwa ajili ya kupokea maoni na kujibu maswali ya Madiwani kuhusu unyanyasi unaofanywa na Migambo kwa wananchi na boda boda.
 Diwani wa Kata ya Itojanda Manispaa ya Tabora Alphonce Shushi  akitoa hoja  jana wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani ya kujadili jinsi Mgambo wanavyopiga na kunyanyasa wananchi wakati wa Doria.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora. Leopold Ulaya akifungua kikao cha Baraza Madiwani jana kilichokuwa kikipitia taarifa za Kata mbalimbali. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Nduguru.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad