Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mercy Mengi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi mjini, kushoto kwa Makamu wa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Anna Mghwira. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Mzee Reginald Mengi mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mercy Mengi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi mjini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro ambaye alikuwa moja ya waliohudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Mercy Mengi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi mjini.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Mzee Reginald Mengi akizungumza na mwanae Bw. Abdiel Mengi wakati wa Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Mercy Mengi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi mjini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Dkt. Maria Kamm (kulia) ambaye alikuwa moja ya waliohudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Mercy Mengi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi mjini.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment