HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 28 November 2018

Kesho ni Usiku wa EUROPA ndani ya StarTimes

Wakati baadhi ya timu kubwa zitakazocheza Europa Alhamisi hii zikiwa tayari zimeshajihakikishia kufuzu hatua ya mtoano, timu nyingine bado zinasuasua. Wawakilishi pekee wa ligi ya Uingereza - Chelsea na Arsenal -  wao tayari wameshajihakikishia kufuzu, lakini AC Milan na Celtic bado hali ni tete, huku mabingwa wa zamani wa Ulaya Olympique Marseille wameshayaaga mashindano hayo.

Arsenal wanahitaji ushindi nchini Ukraine watakapocheza dhidi ya Vorskla Poltava ili waweze kuongoza Kundi E huku wakifuatiwa na Sporting Lisbon bila kujali matokeo ya michezo ya mwisho wiki mbili zijazo. Kocha wa Arsenal Unai Emery anatarajia kuwapumzisha baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza katika mchezo huo, huku mshambuliaji mwenye kiwango bora kabisa Pierre Emerick Aubameyang akitarajiwa kukaa nje pia.

Licha ya Arsenal kujiandaa na mchezo dhidi ya Tottenham wikendi hii, kocha Emery alisisitiza baada ya ushindi wa 2- 1 dhidi ya Bournemouth Jumapili iliyopita kwamba ligi ya Europa ni muhimu sana. “Tunataka kumaliza tukiwa vinara wa kundi (Europa). Ni safari ndefu na ghafla tunacheza na Tottenham, lakini ninataka kuipumzisha timu katika michuano (Europa) hii.
“Tunataka kumaliza tukiwa wa kwanza lakini Jumapili tuna mchezo muhimu sana”

Chelsea wanaofundishwa na Maurizio Sarri wako katika nafasi nzuri zaidi wakiwa wanaongoza kundi mbele ya klabu kutoka Hungary MOL Vidi kwa alama 6 na tofauti ya magoli 5 zaidi. Mechi yao alhamisi hii dhidi ya PAOK ni muhimu zaidi katika kuinua morali ya timu hasa baada ya kupata kipigo chao cha kwanza katika mechi za mashindano msimu huu walipocheza  dhidi ya Tottenham. (Walifungwa na Manchester City pia katika ngao ya hisani lakini ule huwa ni mchezo mmoja tu na sio mashindano). Timu nyingine ambazo tayari zimeshafuzu hatua ya mtoano ni vilabu viwili kutoka Bundesliga Eintracht Frankfurt na Bayer Liverkusen, pamoja na Lazio na Dinamo Zagreb.

AC Milan wanahitaji kushinda mchezo wao dhidi ya Dudelange ili kujihakikishia alama 3 ambazo zitawaweka juu ya Olympique Marseille wanaoshika nafasi ya tatu pamoja na Real Betis katika Kundi F.
Michezo hii yote inaonyeshwa moja kwa moja na chaneli za michezo katika king’amuzi cha StarTimes ambapo wanatakiwa kujiunga na kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 14,000/= tu watumiaji wa dikoda za Antenna na SMART kwa Tsh 21,000/= tu kwa watumiaji wa dikoda za Dish.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad