HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 1 November 2018

KAMATI ZA BUNGE ZAFANYA VIKAO JIJINI DODOMA

 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu hali ya migogoro ya ardhi Nchini katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Taarifa hiyo iliwasilishwa na Kamishna wa Ardhi Ndugu Mary Makondo
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mheshimiwa Nape Nnauye akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo leo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu hali ya migogoro ya ardhi Nchini.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angelina Mabula akifafanua hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo iliyokutana katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu hali ya migogoro ya ardhi Nchini.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma wakiwa katika kikao cha kamati kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo leo walipokea na kujadili taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu Uwekezaji katika Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Mheshimiwa Richard Ndasa akichangia jambo katika kikao cha kamati hiyo  kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo leo walipokea na kujadili taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu Uwekezaji katika Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Mheshimiwa Raphael Chegeni akifuatilia jambo katika kikao cha kamati hiyo  kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo leo walipokea na kujadili taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu Uwekezaji katika Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).Pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo Ndugu Amina.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Mazingira na Utafiti kutoka Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  Ndugu Joseph Kombe akiwasilisha taarifa Kuhusu uhifadhi wa maeneo lindwa pamoja na jitihada za Serikali za kuyahifadhi maeneo hayo mbele ya kikao cha Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Sadiq Murad.

 PICHA NA OFISI YA BUNGE

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad