HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 22 November 2018

Dereva Boda Boda anayekimbiza kwenye Bongo Star Search

“…sikuwa nafahamu, aliniambia usaili unafanyika Club Next Door wahi uende ukajaribu bahati yako huwezi jua. Akaniongezea na Tsh 2000.”

Anaitwa Julius Macha mkazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam ambaye ni miongoni mwa washiriki 17 waliongia katika kambi ya Bongo Star Search jijini Dar es Salaam. Alifanikiwa kufikia hatua hiyo baada ya kupita kwenye usaili wa Dar es Salaam kati ya tar 12 na 14 mwezi Oktoba na kuwa kati ya wawakilishi 10 wa mkoa wa Dar es Salaam.
Julius anaimba muziki wa miondoko ya Rap na ndiye mshiriki pekee kati ya wote 17 wa msimu huu ambaye anafanya hivyo. Anaeleza kuwa amepokelewa vizuri na majaji wote pamoja na mashabiki wa Msimu wa tisa wa Bongo Star Search. 
“Nilipofika kwa majaji sikuwa na uoga nilionyesha kujiamini, nikafanya muziki wangu na wakanikubali nikawa nimepita kwenye top ten ya Dar es Salaam. Siku iliyofuata tukaingia kwenye mchujo wa nchi nzima ambapo nashukuru pia nilifanikiwa kupita na kuingia kwenye kumi na sita bora”, alisema James.
“Siku ya usaili sikuwa nafahamu, nilikuwa naendelea tu na kazi zangu za kila siku. Kuna mama mmoja ambaye ni mteja wangu huwa nambebea mizigo yake kuelekea Coco Beach, tukiwa njiani akaniuliza Vijana wangu huwa wanasema unaweza kuimba, hivi unajua kuna usaili wa BSS unaendelea? aliniambia usaili unafanyika Club Next Door wahi uende ukajaribu bahati yako huwezi jua, nikakubali na akaniongezea Tsh 2000 ya kunisaidia.” Julius
Julius alifika kwenye usaili na pikipiki ambayo anadai sio mali yake, na muda wote alikuwa anatoka nje ya ukumbi wa usaili kwenda kuhakikisha usalama wa chombo hicho cha moto. Kwa sasa Julius anasema ameirudisha pikipiki hiyo kwa mmiliki wake huku akijaribu kuielekea ndoto yake ya kuwa mwanamuziki, na anayo matarajio makubwa kupitia Bongo Star Search atafanikiwa kuifikia ndoto hiyo.
Julius Macha aliperform wimbo ‘Habari ndo hiyo’ wa msanii maarufu wa kizazi kipya Mwana FA na kuvutia wapiga kura wengi ambao hupiga kura kupitia App ya StarTimes ON inayopatikana Play Store na App Store, kwa sasa Julius ndiye anayeongoza kwenye chati za kura. Bongo Star Search inaonekana kupitia chaneli ya ST Swahili kila siku saa 3 Usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad