HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 29, 2018

Chuo cha ustawi wa jamii wawajengea uwezo wa wanafunzi kuelekea mapinduzi ya viwanda

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Eventus Mugyabuso amesema kwa kuelekea mapinduzi ya Viwanda ni fursa ya wasomi kuchangamkia katika fursa ya ajira.Mugyabuso ameyasema hayo leo wakati wa Kongamano la 42 la Chuo  ya kujadili nafasi ya Viwanda kwa wasomi katika kuleta matokeo ya chanya ikiwemo na wao kuwa sehemu ya watu wenye viwanda hivyo.

Amesema kuwa Chuo cha Ustawi wa Jamii kina nafasi kubwa katika kuelekea Sekta ya viwanda kutokana na jinsi elimu wanayoitoa.
Nae Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu Elia Kasile amesema kuwa maarifa  wanayopata katika Chuo cha Ustawi ni nafasi tosha katika kuingia katika Sekta ya viwanda.
Amesema kuwa wahitimu na wanafunzi wanatakiwa kujiamini katika kitu wanachokifanya.
Kasile amesema hakuna kitu kichoweza kushindikana.
 Mhadhiri msaidizi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Prisca Kimario  akizungumza  kuhusiana nafasi ya Viwanda kwa wanataaluma wakati wa warsha ya kujadili sekta ya viwanda kwa wanafunzi na wahitimu wa chuo cha ustawi wa jamii iliyofanyika katika ukumbi wa maktaba wa chuo hicho ,jijini Dar es Salaam leo.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) Elia Kasile akitoa mada kwa wanafunzi na wahitimu wa chuo cha ustawi wa jamii kuhusiana na taaluma wanayoipata kwenda kuchagiza katika sekta ya viwanda wakati warsha ya wahitimu na wafunzi wa chuo hicho uliofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu Elia Kasile akizungumza wakati warsha kwa wanafunzi na wahitimu wa Chuo cha Ustawi wa  jamii  kuhusiana na  elimu wanayipata kuitumia katika sekta ya viwanda iliyofanyika chuuoni hapo leo.
Wanaotarajia kuhitimu Chuo cha Ustawi wa Jamii na wanafunzi wakiwa katika warsha ya kujadili nafasi ya Sekta ya Viwanda kwa wasomi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad