CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 28 November 2018

CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
SERIKALI ya China kupitia ubalozi wake nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es saalam wameandaa semina maalumu ambayo imelenga kujadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na kuimaimarisha masuala ya biashara.

Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo naibu Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya amesema kuwa semina hiyo imeandaliwa na Serikali ya China chini ya ubalozi wa nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya kujenga uhusiano pamoja na kujenga na kuimarisha mahusiano ya kibiashara.

Manyanya amesema kuwa semina hiyo imelenga kupanga mikakati ya kushirikiana baina ya nchi hizo mbili pamoja na faida kwa nchi hizo za Tanzania na China ambazo zimekuwa na uhusiano bora kwa muda mrefu na ameeleza kuwa Tanzania ina rasilimali za kutosha na mahusiano hayo yatasaidia sana katika kufikia malengo ya nchi ya kufikia uchumi wa kati 2025. Amesema kuwa agenda ya viwanda wana malengo ya kuongeza rasimali hasa za kilimo, madini nakadharika.

Pia amesema kuwa semina hiyo ambayo wazawa wanashiriki itakua chachu ya kufungua milango katika sekta ya viwanda. Pia amesema kuwa, "Katika kuwainua wazalishaji (wakulima) tutatoa elimu kuhusiana na masoko na ukuaji wa viwanda nchini na tutahakikisha wanajihusisha na  kilimo chenye tija  na ninawahakikishia kuwa watanufaika  na mikakati inayofuata  na kutambua namna ya kufanya kilimo kitakachowasaidia" ameeleza Manyanya.

Kwa upande wake balozi wa China nchini Wang Ke amesema kuwa mjadala huo utasaidia sana katika kufikia malengo ya nchi ya mwaka 2025 katika uchumi. Na wameandaa semina hiyo kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa lengo la kubadilishana mawazo pamoja na kujadili sera na mikakati katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Wang Ke amesema kuwa Tanzania inahitaji biashara hivyo lazima waangalie namna ya kuimarisha miundombinu ya nchi kavu na baharini na namna ya kufanya hivyo katika sekta ya elimu kwa kutoa ufadhili wa kielimu na mafunzo mbalimbali hivyo wanataka kujadili wa watanzania na kujua mikakati ambayo itawasaidia kusaidia zaidi.

Pia mwakilishi wa Shirikisho la wenye viwanda Afrika (UNIDO)  Dkt. Stephen Bainos amesema kuwa wao kama shirikisho ni kuhakikisha washirika ikiwemo Tanzania wanakua kiuchumi na mkutano huo wa leo ni wakuzidi kujenga mahusiano mazuri pamoja na kubadilishana mawazo na malengo na wao kama shirikisho wanaamini kuwa mkutano huo utatoa matunda bora. Amesema kuwa semina hiyo ni nzuri kwa maendeleo ya viwanda na Tanzania ipo tayari kufanya kazi na China ilikuweza kufikia malengo ya kufikia uchumi wa wa viwanda 2025.
 Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji Mhandisi. Stellah Manyanya akizungumza wakati wa akifungua  semina hiyo iliyoshirikisha wadau wa biashara kutoka Tanzania na China.
Balozi wa China nchini Wang Ke akizungumza  wakati wa semina hiyo ya kuimarisha uhusiano ambapo amesema kuwa wapo bega kwa bega na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha malengo ya kufikia uchumi wa kati 2025 yanafikiwa.
Baadhi wa washiriki wa semina wakifuatilia mjadala huo ambapo wadau mbalimbali wa kiuchumi wamekutana na kubadilishana mawazo juu ya namna bora ya kukuza uchumi.
 Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Stellah Manyanya na Balozi wa China nchini Wang ke wakiwa  kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa biashara wa hapa nchini na kutoka nchini China.
(Picha na Agnes Francis, Blogu ya Jamii.)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad