HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 28, 2018

BENKI YA NBC YACHANGIA DAMU MPANGO WA TAIFA DAMU SALAMA

Na Chalila Kibuda, Blogu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa benki ya  NBC Theobald Sabi amesema kuwa kama wadau wa kijamii na maendeleo wanawajibu wa kuchangia damu kwa wahitaji wa damu kote nchini. Akizungumza wakati wa uchangiaji wa damu  kupitia mpango wa taifa wa damu salama Mkurugenzi mtendaji wa NBC Sabi amesema kuwa watu wenye uhitaji wa damu ni wengi na uchangiaji ni mdogo hivyo wakiwa wafanyakazi wa benki ya NBC wamechangia na wataendelea kuchangia  damu ili iweze kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Amesema kuwa mpango wa taifa wa damu salama damu inayohitajika ni unit 600000 mpango mkakati wao ni kukusanya unit 375,500 kwa mwaka sawa na asilimia70. Kwa upande wake Mkurugenzi wa hazina na masoko ya fedha wa NBC Peter Nalitolela amesema kuwa benki ya NBC kupitia idara yao waliona umuhimu wa kuchangia damu na kushawishi wafanyakazi na wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuchangia damu ambayo itawasaidia watu wenye mahitaji maaalumu.

Ameeleza kuwa wanaendelea kujipanga ili kuhakikisha kila mwaka wanakusanya damu kwa kuwa mahitaji ya damu inayokusanywa haitoshelezi mahitaji. Pia Afisa wa uhamasishaji wa mpango wa taifa wa damu salama kanda ya Mashariki Fatuma Mjungu amesema kuwa wanashukuru benki ya NBC na kuwataka waendelee hivyo hivyo kwani mahitaji ya damu ni makubwa sana.

Na amewataka wadau wengine kujitokeza katika uchangiaji wa damu kwa kuwa mahitaji ya damu ni makubwa sana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Benki hiyo kushiriki katika uchangiaji damu iliyofanyika katika viwanja vya NBC jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa NBC Peter Nalitolela akizungumza kuhusiana na Kitengo chao cha kuratibu uchangiaji damu kutokana na mahitaji kuwa makubwa kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya NBC jijini Dar es Salaam.
 Mwananchi akichangia damu baada ya kuwakuta wafanyakazi wa NBC wakiendelea na uchangiaji damu
 Wafanyakazi wakijisajili kwa ajili ya uchangiaji damu kupitia mpango wa Taifa wa Damu Salama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad