HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 26, 2018

BUNGE SPORTS CLUB YAAHIDI USHINDI MICHUANO YA EALA

Wachezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanaume) Mhe. Aeshi Hillary Mhe. Seif Gulamali na Mhe. David Silinde wakifanya mazoezi Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao.
Mchezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanawake) Mhe. Rita Kabati akipiga mpira wakati wa mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao. Kushoto ni Mhe. Faida Bakari.
Mchezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanawake) Mhe. Neema Mgaya akipiga mpira wakati wa mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao. Kushoto ni Mheshimiwa Rita Kabati. PICHA NA OFISI YA BUNGE.

Na  Mwandishi wetu, Dodoma
TIMU ya Bunge Sport Club imetamba kuvunja mazoea ya timu hiyo kushika nafasi ya pili na kurejea naushindi wa jumla katika michuano ya mashindano ya michezo ya Wabunge  wa Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Desemba mosi mwaka huu Jijini Bujumbura nchini Burundi. Tambo hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na makocha na nahodha wa timu hiyo wakati timu hiyo ikiendelea na mazoezi makali  katika viwanja vya  Jamhuri na CBE Jijini Dodoma.

Mwandishi wetu amefika katika uwanja wa Jamhuri na uwanja wa CBE  asubuhi na kushuhudia timu hiyo ikiendelea na mazoezi makali ambapo kwa upande wa Soka ilikuwa chini ya Kocha Msaidizi ambaye ni Mbunge wa Wawi, Mheshimiwa Ahmed Juma Ngwali. Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kocha Msaidizi wa Timu ya Soka Mheshimiwa Ngwali ameahidi timu yake kuvunja mazoea ya kushika nafasi ya pili na kuahidi kurejea na ushindi.

“Naahidi matokeo mazuri, najua timu nyingi zimejiandaa kwa sababu haya ni mashindano makubwa, mara nyingi imezoeleka timu za Kenya au Uganda ndio zinashika nafasi ya kwanza, mara hii tunaenda kuvunja huo utaratibu lazima sisi tuchukue nafasi ya kwanza” alisema Mheshimiwa Ngwali  Mheshimiwa Ngwali amesema timu hiyo imejifua vya kutosha na wamejitahidi kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika michuano iliyopita.

Kwa upande wa timu ya Mpira wa Wavu inayojifua katika Viwanja vya Chuo cha Biashara CBE Kocha Salum, timu zote za Wanawake na Wanaume wameahidi kufanya vizuri katika michuano hiyo.
 Nahodha wa timu ya Mpira wa Wavu ya Wanaume Mheshimiwa Aeshi Hilary amesema wachezaji wa mpira wa wavu wako vizuri na amewaahidi wabunge na watanzania kwa ujumla kuwa wanaenda kuchukua Ushindi.

Naye Nahodha wa Timu ya Mpira wa Wavu ya Wanawake Mheshimiwa Jesca Kishoa amesema wachezaji wamejipanga kisawaswa kuhakikisha wanarejea nchini wakiwa na ushindi.  Katika mchezo wa Netiboli, Kocha wa timu Netiboli, Eleonora Mongi alisema maandalizi yanaendelea vizuri kwa mchezo huo na wanauhakika wa kutetea ubingwa wa mashindano hayo kutokana na maandalizi ya kueleweka waliyoyafanya.

Timu ya Bunge Sports Club imeweka kambi ya zaidi ya wiki tatu pamoja na kucheza michezo kirafiki ili kuangalia mapungufu ya timu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad