HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 30 November 2018

BENKI YA KCB TANZANIA YANDAA SEMINA ‘BIASHARA CLUB’ KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME).

BENKI ya KCB  nchini  yaendesha kongamano la Biashara Club kwa mara ya pili mwaka 2018 jijini Mwanza,baada ya kongamano  la kwanza likiwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu.

 Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika sekta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.

Semina hiyo iliyofanyika katika jijini Mwanza ilikusanya
wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani, uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo. Nia kubwa ya 
KCB  ikiwa ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba.

Akiongea katika warsha hiyo, Meneja wa Tawi Benki ya KCB Mwanza, Emmanuel Mzava aliwashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa Kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika kukabiliana na changamoto za kibiashara.

 “Mtegemee semina kama hizi kwa siku za mbeleni kwani Mwanza ni jiji linaloonyesha kushamiri kibiashara” aliongezea Mzava.

NayeSwetbert Thomas ambaye ni mtaalamu wa mswala ya kodi aliyealikwa na KCB kwa ajili ya kutoa mafunzo katika warsha hiyo aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muuhimu wa kuelewa mifumo ya kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara zao.

Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua wigo wa biashara zao. KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara
wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia
inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.
 Mkuu wa Kitengo cha wafanyabishara wadogo na wa kati  Abdul Juma akizungumza na wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarihe 29.11.2018. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lento la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
 Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB Lightness May kijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarehe 29.11.2018 jijini Mwanza. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
 Wafanyabiashara wakiwa wanaendelea kufuatilia semina.

Wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiwa katika picha ya pamona wakati wa utambulisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad