HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 3 October 2018

UEFA EUROPA league kuendelea tena Alhamis hii ndani ya Startimes

UEFA EUROPA league itarejea tena usiku wa tarehe 4 ya mwezi Oktoba siku ya Alhamisi kama ilivyo kawaida ya ligi hiyo. Kivutio kikubwa kwa msimu huu kikiwa ni timu kubwa kutoka ligi ya Uingereza (PL) Chelsea na Arsenal ambazo zina mashabiki na wapenzi lukuki katika bara la Afrika na hasa nchini Tanzania.

Kwa wiki hii Arsenal itakuwa ugenini dhidi ya Qarabag FK katika dimba la Baku Olympic Stadium, Arsenal wataingia uwanjani bila kiungo wao Muarmenia Henrikh Mkhitaryan ambaye hataweza kuingia nchin Azerbaijan kutokana na uhasama baina ya nchi hizo mbili. Pia timu hiyo imeshinda mechi zao tano zilizopita katika mashindano yote na wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.

Kwa upande wa Chelsea wao watakuwa nyumbani katika dimba la Stamford Bridge maarufu kama darajani wakiwakaribisha MOL Videoton ya Hungary. Chelsea wamepata matokeo ya kuridhisha tangu kuanza kwa msimu mpya, Eden Hazard anatarajiwa kuendeleza wimbi lake la upachikaji mabao kwa msimu kwani amekuwa na kiwango bora kabisa akiamua matokeo ya mechi kadhaa na za muhimu kwa timu yake.

Mechi kubwa inatarajiwa kuwa ile ya AC Milan dhidi ya Olympiacos katika dimba la Giuseppe Meazza, AC Milan bado hawajawa na makali yao ya zamani lakini wanaonesha kiwango kizuri katika ligi ya Italia, pia watakuwa bila mshambuliaji wao Gonzalo Higuain ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. Mchezo huu utarushwa moja kwa moja kwa lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee.

Michezo mingine ni RB Leipzig dhidi ya Celtic FC, Bayer Leverkusen dhidi ya AEK Larnaca FC, Fenerbahce dhidi ya FC Spartak Trnava, Anderlecht dhidi ya GNK Dinamo Zagreb, michzo yote hii itarushwa moja kwa moja katika chaneli za michezo kwenye king’amuzi cha StarTimes.

Mbali na mechi za EUROPA burudani ya aina yake itakuwa Wikendi hii katika jiji la Paris ambapo vinara wa Ligue 1, Paris Saint German watakuwa nyumbani dhidi ya mahasimu wao Olympic Lyon. PSG wana kikosi bora chenye wachezaji wenye majina na uwezo mkubwa lakini Lyon kikosi chao kinaundwa na Vijana wenye vipaji na uwezo vile vile, itakumbukwa msimu uliopita Lyon waliilaza PSG mabao 3-2 katika dimba hilo hilo. Macho yetu yataelekea Paris wikiendi hii huku mchezo ukiwa mubashara kupitia StarTimes ambao watarusha mechi zote za ligi hiyo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad