HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 6 October 2018

TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION WAIOMBA SERIKALI KUWAPA KIBALI CHA KUANZA KULEA WAZEE KATIKA NYUMBA YA WAZEE ILIYOPO KWEMBE

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
ASASI ya kiraia ya Tushikamane pamoja  foundation imeiomba serikali kuwapa kibali cha kuwaruhusu kuanza kuwatunza wazee katika nyumba ya asasi hiyo iliyopo Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya wazee duniani, Mwanzilishi wa asasi ya kiraia ya Tushikamane pamoja, Rose Mwapachu  amesema kuwa kwa sasa wameshatuma  maombi ya kupata kibali kwaajili ya wazee kukaa katika nyumba waliyoijenga.

"Kwa sasa tumeshatuma maombi serikalini ya kuomba kibali kwaajili ya wazee wasio na ndugu na wasiojiweza kukaa katika nyuma hii tuliyoiandaa kwaajili ya wazee hawa."

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusheherekea siku ya wazee, Rose Mwapachu amesema kuwa nyumba hiyo ni kwaajili ya wazee wasiokuwa na ndugu na wasio na sehemu za kuishi ndio watakao kuja kuishi hapa. 

"Hivyo kwa wazee na wasio na ndugu wala watoto ndio wataishi katika nyumba hii ili kuepusha watu wa madai au kuja kudai mirathi hapa." Amesema Rose Mwapachu.

Kwa upande wa serikali mwakilishi wa  Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo,  Zainabu Mwafilamba amesema kuwa Maombi ya Tushikamane pamoja Foundation tumeyaona na yanafanyiwa kazi.

Na kwa upande wa wazee wasio na makazi na wasio na ndugu jijini Dar es salaam wamewashukuru Tushikamane Pamoja Foundation kwa kuwajali kama wazazi wao.

"Sisi wazee wa Dar es Salam tunawashukuru sana Tushikamane pamoja foundation kwa kutujali sisi wazee Mungua awajalie kila lenye heri watu wote wanaowajali wazee kama sisi".

Pia wamesema kuwa pale tulikuwa na upweke sasa tunajiona kama watuwalio na ndugu kwa mchango wa Tushikamane Pamoja  Foundation wanavyojitoa kwetu.

 Tushikamane pamoja Foundation wamungana pamoja na wazee wasio na makazi jijini Dar es Salaam katika kusheherekea siku ya wazee duniani ambayo  hufanyika duniani kote ifikapo Oktoba 1 kila mwaka.
 Baadhi ya wazee wakielekea katika nyumba ambayo imejengwa na wana tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya kulea wazee wasio na ndugu wala watoto jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wazee wakielekea katika nyumba ambayo imejengwa na wana tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya kulea wazee wasio na ndugu wala watoto jijini Dar es Salaam. 

 Baadhi ya wanatushikamane faundatio wakijumuika na wazee kusheherekea siku ya wazee duniani.
 Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania, Sahabi Isa Gada akiwa amekaa kwenye kitanda kilichopo ndani ya nyumba ya wazee iliyopo Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusheherekea siku ya wazee duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba 1 kila mwaka. Kushoto ni Mwanzilishi wa Tushikamane pamoja Foundationi, Rose Mwapachu.Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania, Sahabi Isa Gada akiwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea  ya nyumba ya wazee iliyopo Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusheherekea siku ya wazee duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba 1 kila mwaka.
Mwanzilishi wa Tushikamane pamoja Foundationi, Rose Mwapachu akizungumza na wazee wakati wa kusheherekea siku ya wazee duniani walipokusanyika leo  katika nyumba iliyojengwa na Tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya wazee.
Baadhi ya wageni waliohudhulia siku ya wazee duniani iliyoandaliwa na Tushukamane pamoja Foundation jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waliofanyikisha jengo la Tushikama pamoja foundation kufikia hii leo.


Baadhi ya wazee.
mwakilishi wa  Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo,  Zainabu Mwafilamba  akizungumza na wazee jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanatushikamane pamoja Foundation wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwakilishi wa wazee akisoma shairi mbele ya wanatushikamane Pamoja Foundation kwaajili ya kuwashukuru.
Keki ya siku ya wazee duniani iliyoandaliwa na Asasi ya kiraia ya tushikamane pamoja Foundation.
Mwanzilishi wa Tushikamane pamoja Foundationi, Rose Mwapachu akishirikiana na wazee kukata keki kwaajili ya kusheherekea siku ya wazee duniani.
Baadhi ya wageni wakiangalia jinsi marazi ya wazee yalivyo.Baadhi ya wazee wakiwa ndani ya chumba mojawapo katika nyumba ya kulelea waze ya kwembe  manispaa ya ubungo jijini Dar es Salaam.


Mwonekano ya nyumba ya wazee iliyopo Kwembe manispaa ya Ubungo iliyojengwa na wanatushikamane pamoja Foundation.
Baadhi ya wazee.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad